Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Natiwa moyo na hatua za utekelezaji wa mkataba wa amani Colombia:Guterres

Natiwa moyo na hatua za utekelezaji wa mkataba wa amani Colombia:Guterres

Pakua

Natiwa moyo na hatua za utekelezaji wa mkataba wa amani nchini Colombia na hususani , kukamilika hapo jana kwa uwasilishaji wa asilimia 30 ya kwanza ya silaha za FARC-EP kwa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Anonio Guterres Alhamisi kupitia taarifa ya msemaji wake, ambayo pia imezichagiza pande zote husika kuendelea kupiga hatua katika mchakato wa utekelezaji wa majukumu yao chini ya mkataba wa amani .

Katibu Mkuu amerejerea kusisitiza kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia mchakato huo wa amani kwa kadri inavyohitajika.

Photo Credit
Kitengo cha Umoja wa Mataifa nchini Colombia cha kukusanya silaha. Picha: UN Mission in Colombia