Ondoeni kizuizi Yemen kuepusha janga la njaa- Mtaalam

Ondoeni kizuizi Yemen kuepusha janga la njaa- Mtaalam

Pakua

Zuio la uingizaji wa bidhaa kwa njia ya anga na majini huko Yemen liondolewe haraka iwezekanavyo ili kuepusha janga la kibinadamu nchini humo.

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu na vikwazo vya kimataifa Idriss Jazairy amesema hayo leo huko Geneva, Uswisi wakati huu ambapo zaidi ya watu milioni 21 nchini Yemen wanahitaji misaada ya dharura ikiwemo chakula.

Amesema zuio hilo lililowekwa mwaka 2015 na vikosi vya ushirika kwenye vita huko Yemen vinakwamisha siyo tu upelekaji wa misaada ya kibinadamu pamoja na vyakula, dawa na mafuta bali pia usambazaji wa kile kinachoweza kuingizwa.

Bwana Jazairy amesema zuio hilo linaenda sambamba na ukiritimba wa kuingia meli kwenye bandari za Yemen akitolea mfano ile ya Al Hudaydah inayotegemewa kwa uingizaji wa asilimia kati ya 80 na 90 nchini humo.

Amezikumbusha pande husika kwenye mzozo huo juu ya haki ya msingi ya kuishi, chakula na maisha ya utu kwa raia wasio na hatia.

Photo Credit
Mtoto nchini Yeman apewa matibabu kwa ajili ya utapiamlo na majeraha. Picha: UNICEF