Skip to main content

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lajadili migogoro barani Ulaya

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lajadili migogoro barani Ulaya

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja António Guterres amewambia wanachama wa baraza la usalama kwamba vita viwili vya kimataifa viliyotokea katika bara la Ulaya kwenye karne ya ishirini ndio mwanzilishi wa Umoja wa Mataifa na baraza hilo na kila  juhudi inahitajika kufanywa kuviepuka.

Bwana Guterres amesema hayo hii leo siku ya Jumanne kwenye kikao cha wazi kilichojadili migogoro barani Ulaya. Amesema japokuwa nchi za Ulaya zimekuwa katika "mstari wa mbele kwa kuzuia vita" katika miaka 70 iliyopita lakini mgogoro huko Georgia mwaka 2008 na ule wa nchini Ukraine mwaka wa 2014 inaonyesha kuwa bara hilo bado liko katika hatari ya kuzuka kwa migogoro mpya.

Katibu mkuu ameongeza kuwa taasisi za Ulaya zimeonyesha ufanisi katika kuunganisha nchi na taratibu za sheria kwa ajili ya kutatua tofauti bila kutegemea ghasia.

(Sauti ya Guterres)

Baraza hili linaelewa migogoro mingi inaendelea kwa sasa barani Ulaya na UM unafanya kazi  kusaidia taasisi hizi kwa kupitia kifungu cha nane cha katiba ya UM. Tunaongoza operesheni za amani katika bara la Ulaya

Bwana Guterres akitaja juhudi za UM ikishirikiana na Umoja wa Ulaya katika maeneo mbali mbali kuleta amani amesema kuna changamoto kama vile kwenye mazungumzo ya kina na ya kudumu kwa ufumbuzi wa suala la Cyprus, Georgia, na Kosovo kupitia azimio 1244, pia  utatuzi wa majina kati ya Macedonia na Ugiriki. Kuhusu mzozo wa sasa Ukraine amesema

(Sauti ya Guterres)

Umoja wa Mataifa unafanya kazi katika juhudi za kuleta amani, utawala bora, haki za binadamu na maendeleo ya kiuchumi, kwa kujiingiza kwa njia tofauti ili kutatua mizozo na kuendeleza amani pia kutilia mkazo michakato ya amani kwenye bara hilo na kwingineko.

Ametaja kuwa migogoro inarudisha maendeleo nyuma na kwamba

(Sauti ya Guterres)

Maendeleo ya kiuchumi yanategemea utulivu na amani ya muda mrefu na kuheshimu haki za binadamu. Hatuwezi kusema kosa moja ambalo limezusha migogoro barani Ulaya bali mikataba ya amani haiheshimiwi na kutekelezwa na mengine ni pingamizi kwa utawala na sheria. Natoa wito kwa sote kuwajibika ikiwa ni pamoja na UM na taasisi za kisheria kufanya juhudi za kutatua mizozo hii na kuleta amani.

Photo Credit
Picha: UN/Rick Bajornas