Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwekeza katika hatua za kijamii ni muhimu katika kutokomeza ukimwi:UNAIDS

Kuwekeza katika hatua za kijamii ni muhimu katika kutokomeza ukimwi:UNAIDS

Pakua

Jumuiya za kijamii zimezitajka nchi wanachama wa Umoja wa mataifa kujumuisha wajibu wa kifedha, huduma na haki kama vipaumbele katika azimio la kisiasa la mwaka 2016 la kutokomeza ukimwi.

Katika majadiliano yasiyorasmi kuhusu ukimwi yaliyofanywa na jumuiya za kiraia na mashirika ya kiraia wamezitaka nchi wanchama wa Umoja wa mataifa kuhakikisha kwamba mapambano dhi ya ukimwi yanafadhiliwa kikamilifu na ufadhili wa hatua za kijamii unaongezwa katika miaka michache ijayo.

Pia wametoa wito kwa watu milioni 30 kupata fursa za dawa za kurefusha maisha ifikapo mwaka 2020 lakini pia kufikia malengo ya kuzuia maambukizi ya virusi vya HIV.

Majadiliano hayo yaliyofanyika makao makao makuu ya Umoja wa mataifa ni sehemu ya mkutano wa ngazi ya juu wa baraza kuu kuhusu kutokomeza ukimwi utakaoanza Juni 8 hadi Juni 10 mwaka huu new York.

Photo Credit
Tangazo hilo litasaidia watoto wachanga wengi kupata matibabu. Picha ya UNAIDS/D. Kembe