Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano DRC yameongeza machungu kwa wanawake:Mratibu

Mapigano DRC yameongeza machungu kwa wanawake:Mratibu

Pakua

Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC mizozo na mapigano Mashariki mwa nchi hiyo vimesababisha siyo tu kupotea kwa maisha ya watu bali pia machungu kwa wale wanaobakia. Jeshi la serikali limekuwa likipambana na waasi na baadhi ya askari wamepoteza maisha huku wengine wakibakia na ulemavu wa maisha na hivyo kushindwa kuendelea na majukumu yao. Matokeo yake wanafamilia wakiwemo wake zao wanalazimika kuwatunza na kulea familia kwa ujumla. Hata hivyo jijini New York, kulifanyika kikao kuona ni vipi teknolojia inaweza kutumiwa kubadili maisha ya watu wanaoishi na ulemavu na miongoni mwa washiriki alikuwa Alain Kashindi Assumani, mratibu wa kitaifa wa mradi wa ujenzi wa Taifa na kuweka utulivu nchini DRC. Bwana Assumani katika mahojiano na Priscilla Lecomte wa idhaa hii alianza kwa kueleza lengo la mkutano .

Photo Credit
Baadhi ya askari waliopata ulemavu wakiwa na wake zao. (Picha:Kwa hisani ya Allain K. Assumani)