Mcheza filamu avunja ukimya kuhusu ukatili wa kingono uliomsibu

Mcheza filamu avunja ukimya kuhusu ukatili wa kingono uliomsibu

Pakua

Mwanamke mmoja kati ya watatu duniani kote amekumbwa na ukatili wa kijinsia! Ukatili huo ni pamoja na kupigwa, kubakwa na hata kunajisiwa wakati akiwa utotoni. Takwimu hizo ziliwekwa bayana wakati wa tukio lililofanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa la siku ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake duniani. Tukio hilo lilishuhudia wageni wakiwa wamevalia mavazi yenye rangi ya chungwa, rangi ya matumaini na kusababisha rangi hiyo kutamalaki ndani ya ukumbi huo. Je nini kilijiri zaidi? Basi ungana na Amina Hassan kwenye makala hii.

Photo Credit
Muigizaji mashuhuri wa filamu nchini Marekani Teri Hatcher wakati akitoa ushuhuda wake. (Picha:UN Women/Ryan Brown)