Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sikufahamu jinsi ya kuzungumza na mwanangu kumuepusha na mimba za utotoni - Mzazi Haiti

Sikufahamu jinsi ya kuzungumza na mwanangu kumuepusha na mimba za utotoni - Mzazi Haiti

Pakua

Hebu fikiria kutarajia kupata mtoto wakati ambapo hata hufahamu neno ujauzito lina maana gani. Hicho ndicho kilichomfika mtoto mwenye umri wa miaka 14 nchini Haiti ambaye alijikuta anapewa ujauzito na kaka wa rafiki ya kiume wa rafiki yake. Hakuwa anajitambua akakubali kumsindikiza rafiki yake na zaidi ya yote akakubali urafiki na kijana huyo mwenye umri wa miaka 16. Mama yake binti huyu naye anasema hakufahamu ni kwa jinsi gani azungumze na mtoto wake ili kumuepusha na uhusiano na wavulana kwa lengo la kumuepusha kupata ujauzito. Maji yameshamwagika hayazoleki lakini shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya watu, UNFPA nchini Haiti linachukua hatua kutoa eliu ya viungo vya uzazi na afya ya uzazi kwa wasichana na watoto wa kike ili kuepusha maji kumwagika zaidi ilhali hayazoleki. Simulizi ya mtoto huyo na kinachofanyika kuwasaidia ndio makala yetu ya leo inayoletwa kwako na Assumpta Massoi.

Audio Credit
Anold Kayanda/Assumpta Massoi
Audio Duration
4'17"
Photo Credit
© UNOCHA/M. Minasi