Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Licha ya mashambulizi bado kuna matumaini ya ujenzi wa taifa Somalia

Wiki hii kiasi cha Euro bilioni 2.4 zimeahidiwa katika kongamano liitwalo New Deal kuhusuSomalia, linayofanyikaBrussels. Ijapokuwa kumekuwa na changamoto, Hatua zimepigwa chini ya Serikali inayoongozwa na rais Hassan Sheik Mohamud , hususani kukuza uchumi wa taifa hilo ambalo limeshuhudia mapigano kwa takribani miongo miwili. Je ninini mustskabali wa Somalia?

Ungana na Joseph Msami katika ripoti hii itakayo kupa jawabu

UNICEF, Ethiopia wapunguza vifo vya watoto

Zikiwa zimesalia chini ya siku 1000 kufikia ukomo wa malengo ya maendeleo ya mileni mwaka 2015, nchi kadhaa zinahaha kutimiza malengo hayo manane yaliofikiwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 2000.

Makala ifuatayo inaangazia namna Ethiopiailivyopiga hatua katika kupunguza lengo la nne

la kupunguza vifo vya watoto walioko chini ya umri wa miaka mitano.

Ungana na Joseph Msami.

UNICEF na washirika wakwamua afya za watoto Uganda

Huduma ya afya ni miongoni mwa changamoto katika nchi zinazoendelea mathalani barani Afrika nchiniUganda. Lakini sasa mambo ni tofauti vijijini ambapo serikali na wadau wa sekta hiyo wakiwamo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF wameleta mabadiliko.

Ungana na Asumpata Masoi kwa undani wa taarifa hii

ICC yazungumzia mpango wa Kenya kutaka kujitoa

Kesi inayaowakabili viongozi wa serikali yaKenyaakiwemo Naibu Rais William Rutto pamoja na mtangazaji wa radio Joshua Arap Sang imeanza kusikilizwa huko The Hague nchini Uholanzi.

Kesi hiyo yenye mvuto nchiniKenya, Afrika mashariki, na dunia nzima kwa ujumla inahusisha tuhuma za kuhusika na vurugu baada ya uchaguzi mkuu nchiniKenya mwaka 2007 ambapo zaidi ya watu 1200 walipoteza maisha huku wengine wakipoteza makazi.

Somalia yaungana kutokomeza vikundi hatarishi

Siku chache baada ya kushuhudiwa milipuko ya mabomu nchiniSomalia, bado matumaini ya kupambana na vikundi vyenye misimamo mikali na uhusiano na ugaidi yapo nchini humo.

Ripoti yua Joseph Msami inamulika juhudi za nchi hiyo katika kusaidia kumaliza chuki na uhasama huo uliogharimu taifa ahilo kwa miongo kadhaa. Ungana naye.

Sababu za watu kujiua zaainishwa

Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kupinga vitendo vya kujiua mwandishi wa idhaa hii kutoka Nairobi Jason Nyakundi amefanya mahojiano na Dk Fredrick Owit kuhusu sababu za watu kujiua pamoja na kukusanya maoni ya wananchi jijini humo.

Ungana naye katika taarifa ifuatayo yenye ufafanuzi zaidi

Biashara zaimarika Somalia

Barabara za Mogadishu zilijulikana kama hatari zaidi kote duniani, zilkuwa ni mahali ambako kulishudiwa ghasia siku nenda siku rudi lakini nyakati zimebadilika na hali imebadailkia pia kwani sasa biashara zinaweza kuendeshwa hapa basi ili kujua hali ilivyo Mogadishu ungana na Joseph Msami