Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

Picha: ©Shutterstock/UNESCO

Ushairi unatupatia matumaini katika wakati huu mgumu-UNESCO

Ushairi unatupa matumaini limesema shirika la Umoja wa mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO, katika kuadhimisha siku ya ushairi duniani , likipongeza uwezo wa aya kutupumzisha na misukosuko ya maisha ya kila siku na kutukumbusha uzuri wa wale wanaotuzunguka na muhimili utu wa pamoja.

Katika ujumbe maalumu wa siku hii mkurugenzi mkuu wa UNESCO Irina Bokova akinukuu utenzi wa mshairi Henry Wadsworth Longfellow amesema

Hatuna mabawa , hatuwezi kuruka

Lakini tuna miguu ya kutembea na kukwea

Maisha ya watu chupuchupu kwenye ajali ya ndege Wau-UNMISS

Mpango wa Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini UNMIS leo Jumatatu umesaidia kunusuru maisha ya watu baada ya ndege iliyokuwa na abiria 43 kuanguka  kwenye uwanja wa ndege wa Wau na kulipuka.

Ofisi ya UNMISS Wau ilikimbiza timu ya dharura kusaidia operesheni za ukozi, ikwa na madaktari, na askari wa zimamoto. Waloshuhudia wamesema ndege hiyo ya shirika la ndege la South Supreme ilikuwa ikijaribu kutua , iliposerereka nje ya mkondo na kushika moto.

Kamati yahaki za watu wenye ulemavu kuwa na mwanamke mmoja tu si sahihi

Ukweli kwamba kuna mwanamke mmoja tu aliyechaguliwa na nchi wanachama kufanya kazi kwenye kamati ya haki za watu wenye ulemavu kimsingi sio sawa.

Huo ni ujumbe bayana uliowasilishwa na naibu kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Kate Gilmore katika ufunguzi wa kikao cha 17 cha kamati hiyo mjini Geneva, Uswisi.

Amezungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliyeliweka suala la usawa wa kijinsia katika uwakilishi wa wanawake kama kitovu cha uongozi wake .

Watu wa asili wana ujuzi na ukizingatiwa utakuza kipato: Mshiriki CSW61

Katika zama hizi ambazo ajira ni changamoto ya kimataifa, jamii ya watu wa asili na ujuzi wao asilia wanaweza kukuza ajira, amesema Lucy Mulenkei kutoka mtandao wa taarifa kwa watu wa asili IIN, nchini Kenya. Bi. Mulenkei anashiriki mkutano wa kamisheni ya hadhi ya wanawake CSW61 mjini New York Marekani. Katika mahojiano na Joseph Msami wa idhaa hii, mshiriki huyo amesema watu wa asili hawanufaikiipasavyo kutokana na kuachwa nyuma na mfumo wa maisha, na kuzisihi serikali kuzitizama jamii hizo alizosema zina ujuzi ambao haujathaminiwa ipasavyo.

UNHCR yalaani kushambuliwa kwa meli huko Yemen

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, limeshutumu kitendo cha kushambuliwa kwa meli moja iliyokuwa imebeba watu takribani 145 karibu na pwani ya Hudaydah nchini Yemen.

Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amewaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo la Alhamisi lilisababisha vifo vya watu 42, miongoni mwao wakimbizi wanawake na watoto.

Amemnukuu Kamishna Mkuu wa UNHCR Filipo Grandi akitoa wito kwa pande husika kuwajibisha wahusika na kuhakikisha tukio kama hilo halitokei tena.

(Sauti ya Farhan)

ILO na wakfu wa Walk Free kuvalia njuga utumwa wa kisasa

Shirika la kazi duniani ILO na wakfu wa walk Free watashirikiana kutafiti kiwango cha utumwa wa kisasa duniani .Katika ushirika huo uliotangazwa mwishoni mwa wiki, mashirika hayo mawili yataanzisha makadirio ya pamoja ya utumwa wa kisasa kwa nia ya mchakato wa kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDGs, huku yakijiwekea kiwango cha asilimia 8.7.

Makadirio hayo ya kimataifa yatakayotokana na mahojiano mbalimbali ya ana kwa ana, yatatoa mwangaza zaidi ya idadi ya walio katika utumwa huo wa kisasa, katika kanda, umri na jinsia.

Mkutano wa 61 wa kamisheni ya hadhi ya wanawake CSW61 waangaziwa

Mkutano wa 61 wa kamisheni ya hadhi ya wanawake umeanza tarehe 13 mwezi huu wa Machi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Asasi za kiraia kutoka sehemu mbalimbali zinazojihusiha na masuala ya ustawi wa wanawake zimewakilishwa huku pia serikali zikituma wawakilishi wake kushiriki katika mikutano mbalimbali ya ndani kuhusu masuala ya wanawake. Je nini kilijiri?

Ijapokuwa hali ya usalama bado ni tete CAR, maendeleo makubwa yamepatikana-Onanga

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) na mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MINUSCA, Parfait Onanga-Anyanga, amesema japokuwa hali ya usalama bado ni tete, lakini maendeleo makubwa yamepatikana tangu tangu uchaguzi wa serikali mpya mapema mwaka jana. Akihojiwa na redio ya Umoja wa Mataifa, Bwana Onanga-Anyanga amesema..

(Sauti ya Onanga-Anyanga)

Wahamiaji wa Guinea waliokwama Libya warejea nyumbani-IOM

Wahamiaji 98 raia wa Guinea wakiwemo wanaume 96 na wanawake wawili waliokuwa wamekwama Libya sasa wamerejea nyumbani Conakry kwa msaada wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM.

Ndege ndogo iliyoandaliwa kwa uratibu wa serikali ya Libya na uongozi wa Guinea iliondoka uwanja wa ndege wa Mitiga tarehe 14 mwezi huu, huku shirika la IOM likifanya usaidi wa safari, uchunguzi wa afya na kutoa msaada mwingine kama mavazi na viatu.