Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

Yemen yazidi kutwama- Baraza

Hali nchini Yemen inazidi kuwa mbaya na ya machungu huku raia wakilipa gharama ya mapigano yanayoendelea kwa miaka miwili sasa.

Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi huu wa Machi, Balozi Matthew Rycroft wa Uingereza amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari hii leo baada ya kikao cha faragha cha baraza hilo kilichoangazia Yemen.

Watu milioni 27 katika nchi nne za Afrika hawana maji safi na salama- UNICEF

Uhaba wa maji, ukosefu wa huduma za kujisafi na tabia zisizo sahihi za kujisafi zinaongeza tishio kwa watoto ambao tayari wanakabiliwa na unyafuzi huko kaskazini-mashariki mwa Nigeria, Somalia, Sudan Kusini na Yemen.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema hayo hii leo likiongeza kuwa takribani watu milioni 27 katika nchi hizo nne zilizo katika tishio la njaa kali wanatumia maji yasiyo safi na salama, jambo linaloweza kusababisha wapate kipindupindu, watoto wakiwa hatarini zaidi.

Raia wengi wameuawa kwenye ukombozi Mosul: Zeid

Wito umetolewa hii leo kwa vikosi vya ulinzi na usalama nchini Iraq kuchukua "tahadhari kubwa"iwezekanavyo katika kampeni zao za kuikomboa Mosul kutoka kwa wanamgambo ISIL huku kukiwa na taarifa kwamba mamia ya raia wameuawa katika mashambulizi ya anga.

Ombi hilo limetolewa na ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa baada ya mashahidi kuelezea kuwa waasi wenye msimamo mkali waliwalilazimisha kukaa katika nyumba zao wakishambuliana na majeshi ya serikali.

Vimbunga Matthew na Otto vyastaafishwa: WMO

Ni kawadia kusikia watu wakistaafu baada ya kufuikia umri fulani kwa mujibu wa sheria za nchi!

Hii imekuwa tofauti kwa binadamu, vimbunga Mathew na Otto ambavyo vimesababisha madhara makubwa yakiwemo vifo na uharibifu wa mali na pia madhara ya kiafya, vimestaafishwa rasmi leo na shirika la kimataifa la hali ya hewa WMO.

Majina ya vimbunga hivyo yamestaafishwa rasmi leo baada ya kusababisha majanga makubwa kwa mwaka 2016  Martin inachukua nafasi ya Mathew na Owen badala ya Otto. Huu ni utaratibu wa shirika hilo wa kutoa majina kwa vimbunga.

UN Photo/Mark Garten)

Nyukilia itumike kwa maendeleo sio silaha-Tanzania

Tanzania imesema inaunga mkono maendeleo ya teknolojia ya nyuklia katika kutibu magonjwa yasiyoambukiza kama vile saratani na utunzaji wa chakula dhidi ya uharibifu, lakini ikasisistiza kwamba matumizi ya silaha za nyukilia ni jinamizi kwa kila mmoja.

Hiyo ni sehemu ya tamko la serikali ya nchi hiyo katika mkutano uliofanyika hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, uliolenga mazungumzo ya kuanzisha chombo cha kisheria cha kupiga marufuku silaha za nyuklia.

UNODC, Kenya wazindua muongozo wa kukabalina na ugaidi.

Ikiwezeshwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya dawa na uhalifu UNODC, serikali ya Kenya kupitia ofisi ya mwendesha mashtaka wa serikali, leo wamezindua muongozo wa kuzingatia haki za binadamu na kushugulikia uhalifu wa kigaidi nchini humo.

Hatua hii ni sehemu ya juhudi za mkakati wa Umoja wa Mataifa wa kukabliana na ugaidi duniani, unaosisitiza jukumu muhimu la kuheshimu haki za binadamu na utawala wa kisheria ikiwamo kulinda haki za wahanga wa ugaidi.

Ndoto za wananchi wa Sudan Kusini kuwa taifa lao huru litaimarika

Kuanzia tarehe 26 hadi 27 mwezi huu wa Machi, Mwenyekiti mpya wa kamisheni ya Muungano wa Afrika, AU Moussa Faki Mahamat alikuwa ziarani nchini Sudan Kusini kujionea hali halisi wakati huu ambapo janga la kibinamu linazidi kupanuka, ikiwa ni zaidi ya miaka mitatu tangu mzozo wa wenyewe kwa wenyewe uibuke nchini humo. Ndoto za wananchi kuwa taifa lao huru litaimarika na kuchanua, zimetumbukia nyongo huku mapigano yakishika kasikila uchao na watoa misaada nao wakiwindwa. Je nini amejionea Bwana Mahamat, katika ziara yake ya kwanza tangu achaguliwe kuongoza kamisheni ya AU?

Surua yashambulia kwa kasi Ulaya: WHO

Kama ulifikiri surua inashambulia bara Afrika pekee, lahasha! Shirika la afya ulimwenguni WHO linasema zaidi ya visa 500 vimeripotiwa barani Ulaya ifikapo jana Januari 27 huku ugonjwa huo unaoathiri watoto ukidaiwa huenda ukisasabisha mlipuko mkubwa zaidi kutokana na kupungua kwa chanjo kwa asilimia 95.

WHO inasema katika taarifa yake ya leo kwamba kwa kipindi cha miaka miwili kiwango cha surua kimeongezeka barani humo na kuongeza kuwa ikiwa kiwangco stahiki cha chanjo hakitafikiwa, ugonjwa huo utaendelea barani Ulaya na kwingineko.

UNICEF na wadau wasaidia zaidi ya 145,000 kwenye baa la njaa Sudan kusini:

Mwezi mmoja tangu kutangazwa kwa baa la njaa katika baadhi ya sehemu nchini Sudan kusini , shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, kwa pamoja na lile la mpango wa chakula WFP na washirika wengine wamefikisha msaada wa kuokoa maisha kwa watu 145,000 wakiwemo watoto 33,000 wa chini ya umri wa miaka mitano.

Timu ya dharura ya watu 13 imepelekwa jimbo la Unity ambako zaidi ya watu 10,000 wanaishi katika kata mbili zilizokumbwa na baa la njaa.