07 Machi 2024
Hii leo jaridani tunaangazia miradi inayotekelezwa na Umoja wa Mataifa huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo -DRC kusaidia wanawake ikiwa ni kuelekea siku ya wanawake duniani hapo kesho Machi 8.
Wanawake na wasichana wakiwezeshwa jamii zinanufaika - Wanabiashara Kenya
Wiki hii Ijumaa tarehe 8 Machi 2024, ulimwengu utaadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambapo mwaka huu ina maudhui “Wekeza kwa wanawake: Harakisha maendeleo,” lakini Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN Women linasema ni dhahiri kwamba ulimwengu bado unakabiliwa na migogoro mingi
Mtoto Charles: MONUSCO imenitoa msituni, asanteni sana
Harakati za ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, za kuondoka nchini humo zikiendelea, tunamulika hatua chanya zilizochukuliwa na ujumbe huo katika kunusuru vijana waliokuwa wanatumikishwa na waasi mashariki mwa nchi hiyo.
WFP/UNICEF: Janga kubwa la njaa duniani linanyemelea Sudan miezi 11 baada ya kuzuka vita
Takriban miezi 11 tangu majenerali wapinzani watangaze vita nchini Sudan, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa leo walionya kwamba mzozo huo unaweza kusababisha janga kubwa zaidi la njaa duniani.
Mchango wa wanawake katika kulinda mazingira ni wa thamani sana: Dkt. Josephine Ojiambo
Katika kuelekea siku ya wanawake duniani ambayo itaadhimishwa Ijumaa wiki hii Machi 8 mchango wa wanawake katika kulinda na kuhifadhi mazingira umeelezwa kuwa ni mkubwa na wa thamani sana.
UN inaonya kwamba vita ya Gaza yaweza kuchochea machafuko zaidi ya kikanda
Mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza yanaendelea nchini Misri kwa siku ya pili leo huku Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa akionya kwamba vita ya Gaza iko katika hatari ya kubadili mweleko na kupanua wigo zaidi utakaoathiri kila nchi Mashariki ya Kati na kwingineko.