Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

05 MACHI 2024

05 MACHI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada ambayo inaangazia jitihada za taasisi ya ProjeKt Inspire ya nchini Tanzania katika kuhamasisha masomo ya STEM yaani Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za Gaza, haki za binadamu, ukulima na usawa wa kijinsia. Mashinani tukielekea siku ya wanawake duniani tutakupeleka katika kaunti ya Kajiado nchini Kenya. 

  1. Baada ya kukosa vibali vya kuingia eneo la Gaza Kaskazini tangu katikati ya mwezi Januari mwaka huu, hatimaye shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limefanikiwa kuingia eneo hilo na kujionea hali ya wananchi na mahitaji ya afya yalivyo pamoja na kupeleka misaada ikiwemo vifaa vya matibabu na mafuta ya kuendeshea mitambo ya hospitali.
  2. Huko Geneva Uswisi mkutano wa 55 wa Baraza La Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu umeendelea leo ambapo Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu biashara na unyanyasaji wa kingono wa watoto Mama Fatima Singhateh ametaka kutambulika kwa hatua za mtu mmoja mmoja au za pamoja za kupambana na unyanyasaji wa kijinsia na unyonyaji wa watoto katika tasnia ya burudani na vyombo vya habari ili kukomeshwa unyanyasiji huo mara moja. 
  3. Na tukiwa katika mwezi wa Machi unaoadhimisha siku ya wanawake duniani shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limezitaka nchi kuhakikisha zinashughulikia changamoto za usawa wa kijinsia kwenye kupambana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi kwani takwimu zinaonesha kuwa familia hususan za vijijini zinazoongozwa na wanawake zinaathirika zaidi na mabadiliko ya tabianchi ikilinganishwa na zile zinazoongozwa na wanaume.
  4. Na mashinani Jane Kamenya, Mama wa watoto wawili na mfyanyabiashara ya usukaji nywele kutoka kaunti ya Kajiado nchini Kenya ambaye kando na kupata manufaa na kuweza kujikwamua kiuchumi yeye anatoa wito kwa vijana na kinamama wajiunge naye katika jukumu muhimu ya wanawake la kuhakikisha jamii zao wameondokana na umaskini.

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
11'24"