Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake na wasichana wakiwezeshwa jamii zinanufaika - Wanabiashara Kenya

Wanawake na wasichana wakiwezeshwa jamii zinanufaika - Wanabiashara Kenya

Pakua

Wiki hii Ijumaa tarehe 8 Machi 2024, ulimwengu utaadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambapo mwaka huu ina maudhui “Wekeza kwa wanawake: Harakisha maendeleo,” lakini Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN Women linasema ni dhahiri kwamba ulimwengu bado unakabiliwa na migogoro mingi, kuanzia mizozo ya kijiografia hadi viwango vya umaskini vinavyoongezeka, ukosefu wa usawa na kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kwa kuwekeza kwa wanawake, tunaweza kuibua mabadiliko na kuharakisha mpito kuelekea dunia yenye afya, usalama na usawa zaidi kwa wote. Nchini Kenya tunakutana na mama mjasiriamali ambaye alianza kwa kufanya kazi na shirika lisilo la kiserikali liitwalo Sime Food, ambalo linahusika na kilimo endelevu, lishe bora, na stadi za biashara ndogo ndogo ili wawe na maarifa na ujuzi unaohitajika ili kupatia familia zao lishe bora mwaka mzima na kuuza masalio ili kusaidia kulipia mahitaji mengine ya kaya. Baada ya kupata mafunzo hayo na fedha za kuanzisha biashara zake, Lucy anachochea kinamama na vijana wa kike wajiunge naye katika sekta ya biashara ili waweze kujikwamua kiuchumi. Selina Jerobon wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amefuatilia na kutuandalia makala hii.

Audio Credit
Anold Kayanda/Selina Jerobon
Audio Duration
4'19"
Photo Credit
UN News