Mamilioni ya watu hawana sehemu ya kunawia mikono-UNICEF
Ingawa kunawa mikono kwa sabuni ni muhimu katika mapambano dhidi ya magonjwa ya kuambukiza ikiwemo COVID-19, mamilioni ya watu duniani hawana mahali pa kunawia mikono, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF katika siku ya kimataifa ya kunawa mikono hii leo.
Ufisadi ni mbaya zaidi hususan wakati wa migogoro-Guterres
Ufisadi ni uhalifu, ukiukaji wa maadili na usaliti wa hali ya juu kwa imani ya umma amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika taarifa yale iliyotolewa leo kuhusu ufisadi na janga la corona au COVID-19.
15 OKTOBA 2020
Jaridani na Flora Nducha pata habari, makala na mashinani
UNICEF na Canada washirikiana kuhakikisha upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa hospitalini
Nchini Haiti, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kwa ufadhili kutoka Canada, wanaanzisha mradi wa kusogeza karibu na makazi ya wananchi huduma za usajili wa watoto ili wapatiwe vyeti vya kuzaliwa katika taifa hilo ambalo mtoto mmoja katiya 6 hana cheti cha kuzaliwa
Wakimbizi wachangai katika kukabiliana na athari za COVID-19 Afrika Kusini
Nchini Afrika Kusini, jamii ya wakimbizi wa Kisomali wameamua kushirikiana na majirani zao raia wa Afrika Kusini kuwasaidia watu ambao wanahangaika na maisha katika kipindi hiki cha janga la COVID-19 nchini humo.
Vijana Uganda wakaribisha sheria ya kugombea chini ya umri wa miaka 30.
Kwa miaka 25 ya katiba ya Jamhuri ya Uganda, vijana walio chini ya umri wa miaka 30 wamekuwa wakisaka fursa ya kukubaliwa kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa katika serikali za mitaa kutokana na vizuizi vya sheria za uchaguzi.
Hatua zinahitaji kuwekwa kuhakikisha malengo ya kuzuia na kutibu TB yanafikiwa
Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO imeonya kwamba endapo uwekezaji na hatua za haraka hazitochukuliwa malengo ya kuzuia na kutibu kifua kikuu au TB huenda yasitimie mwaka 2022.
14 Oktoba 2020
Ungana na Flora Nducha katika jarida kwa habari, makala na mashinani
Ari ya watoto wakimbizi kutaka kusoma inanipa motisha kufundisha
Kutana na mwalimu kutoka nchini Uturuki anayesema janga la corona au COVID-19 lilimvunja moyo na kumkatisha tamaa, lakini ari ya wanafunzi wake ambao asilimia kubwa ni wakimbizi kutoka kutoka Syria ilimpa nguvu ya kuendelea kufundisha.