COVID-19 ni madhila juu ya madhili kwa watoto DRC
Mfumo wa afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, unahitaji msaada wa haraka wakati huu ukilemewa na magonjwa ya surua na kipindupindu yanayokatili maisha ya maelfu ya watoto pamoja na tishio la janga jipya la virusi vya Corona COVID-19. Jason Nyakundi na maelezo zaidi.
31 Machi 2020
Assumpta Massoi : Hujambo na Karibu kusikiliza Jarida kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, kutoka hapa New York Marekani.
JINGLE (04”)
ASSUMPTA:Ni Jumanne ya Machi 31 mwaka 2020, mwenyeji wako studioni hii leo ni mimi ASSUMPTA MASSOI
COVID-19: Kutembea usiku sasa ni hatia Uganda
Uganda imefuata nyayo ya baadhi ya nchi duniani ya kupitisha amri ya kutotembea usiku kama mojawapo ya njia za kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19, sanjari na kufunga mipaka yake na kupiga marufuku usafiri wa magari binafsi.
Kampuni ya ZuRi Africa yajitosa kusaidia harakati dhidi ya COVID-19 Tanzania
Kutokana na kuendelea kusambaa kwa virusi vya ugonjwa wa Corona, COVID-19, maeneo mbalimbali duniani, Umoja wa Mataifa umekuwa ukisihi wadau kujitokeza kuunga mkono hatua za kimataifa na kitaifa za kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo visivyo na tiba wa
Mradi wa kutengeneza sabuni ni mkombozi kwa wanawake wakimbizi Za'atari
Kwa kutumia bidhaa za asili, wanawake wakimbizi kwenye kambi kubwa zaidi nchini Jordan wanatengeneza sabuni na kugawa kwa familia zilizo na mahitaji kwa ajili ya kusaidia katika kuzuia kuenea kwa virusi vya corona au COVID-19. Jason Nyakundi na taarifa zaidi
Kijana atumia ubunifu kutengeneza kitu cha kusafi mikono, vita dhidi ya COVID-19
Ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19 ukiwa umeshasambaa katika mataifa 199 ikiwemo Tanzania ambako hivi sasa idadi ya wagonjwa imefikia 19, vijana nao wanaibuka na ubunifu mbalimbali ili kusaidia mataifa yao katika kudhibiti kuenea kwa gonjwa hilo lisilo na tiba wala chanjo.
30 Machi 2020
Assumpta Massoi : Hujambo na Karibu kusikiliza Jarida kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, kutoka hapa New York Marekani.
JINGLE (04”)
ASSUMPTA:Ni Jumatatu ya Machi 30 mwaka 2020, mwenyeji wako studioni hii leo ni mimi ASSUMPTA MASSOI
ILO na UNICEF yatoa mapendekezo ya namna ya waajiri kusaidi familia waajiriwa na familia zao
Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa, lile la kuhudumia watoto, UNICEF na lile la kazi, ILO leo wametoa mapendekezo ya jinsi waajiri wanaweza kusaidia waajiriwa na familia zao wakati huu wa janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19. Flora Nducha na ripoti kamili.
Wakimbizi wakosa mgao wa chakula kufuatia marufuku ya usafiri wa umma, Uganda
Nchini Uganda kama ilivyo katika maeneo mengine duniani imeimarisha hatua za kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa wa Corona au COVID-19 kutokana na ongezeko la wagonjwa.