Janga kubwa la kibinadamu linanyemelea Tanganyika, DRC
Janga kubwa la kibinadamu linanyemelea maeneo ya kusini-mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wakati huu ambapo eneo hilo linakumbwa na mapigano na ukiukwaji mkubwa wa kibinadamu. Limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.