Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Janga kubwa la kibinadamu linanyemelea Tanganyika, DRC

Janga kubwa la kibinadamu linanyemelea Tanganyika, DRC

Pakua

Janga kubwa la kibinadamu linanyemelea maeneo ya kusini-mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wakati huu ambapo eneo hilo linakumbwa na mapigano na ukiukwaji mkubwa wa kibinadamu. Limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi,  UNHCR

Huyu ni Jean Kiza Kambi, mmoja wa wakimbizi wa ndani aliyesaka hifadhi katika kituo cha kuhifadhi wakimbizi wa ndani cha Kalunga, karibu na Kalemie, mji mkuu wa jimbo la Tanganyika nchini DR Congo. Hali si shwari kwenye eneo lao, simulizi ya mapigano ya kikabila baina ya makabila ya Twa, Luba na mengineyo.

(Sauti ya Jean Kiza Kambi)

Nyuso za wanawake ni za kukata tamaa zikidhihirisha machungu waliyopitia. Marie Seluwa Makelo ni mmoja wao..

(Sauti ya Marie Seluwa Makelo)

Mwaka 2017 pekee UNHCR na wadau wake wameripoti visa 12,000 vya ukiukwaji wa haki za binadamu kwenye jimbo la Tanganyika na maeneo ya jirani ya Pweto yaliyoko jimbo la Katanga Juu.

Andrej Mahecic ni msemaji wa UNHCR, Geneva, Uswisi.

(Sauti ya Andrej Mahecic)

“UNHCR inatoa tiwo kwa mamlaka za DR Congo zihakikishe ulinzi wa raia na kufuatilia kwa makini ripoti za uhalifu uliofanywa na jeshi na vikundi vilivyojihami na kuachana na fikra ya ukwepaji sheria kwa wakiukaji wa haki.”

Pamoja na wito wa kutaka haki itendeke, Bwana Mahecic amerejelea wito wa UNHCR wa ombi la zaidi ya dola milioni 368 kwa mwaka huu wa 2018 ili kushughulikia janga la kibinadamu linalokumba DR Congo.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
1'44"
Photo Credit
Wanawake nchini DRC. (Pichay © MONUSCO Myriam Asmaniy)