Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutana na mtawa anayebadili maisha ya maelfu ya wanawake DRC

Kutana na mtawa anayebadili maisha ya maelfu ya wanawake DRC

Pakua

Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo- DRC- wanawake wanapitia madhila makubwa kutokana na vita vya muda mrefu vinavyoendelea na kuwaacha wanawake na watoto katika taharuki. Lakini mtawa mmoja , Angelique amedhamiria kufuta machozi yao.

Akiwa mitaani na baiskeli yake na dhamira ya ukombozi, mtawa sista Angeligue anatambua kuwa maelfu ya wanawake wameepuka  kutekwa, kuteswa na unyanyasaji wa kingono na anataka kubadili fikra hizo na kuwapa matumaini.

(Sauti ya Sista Angelique)

 “Ninapowaona wanakuja toka msituni wakiwa wametawanywa na kukimbia zahma , nyuso zao zinaonekana tofauti kabisa.”

Sasa Sista Angelique anawasaidia wanawake hao manusura kujenga upya maisha yao kwa kuwafundusha kusoma na kuandika , na kwa kuwapa mafunzo hayo anawasaidia kujitegemea.

(Sauti ya Sista Angelique)

“Endapo nitaweza kumsaidia hata mwanamke mmoja tu kuanza upya maisha yake kwangu mimi hayo tayari ni mafanikio, kamwe sitokata tamaa.”

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema Sista Angeleque kwa kufanya hivyo anatuma ujumbe mzito kwamba wanawake ni wastahimilivu na wanaweza kukabili lolote.

Audio Credit
Patrick Newman
Audio Duration
1'20"
Photo Credit
Bango linalosisitiza umuhimu wa kupinga na kutokomeza unyanyasaji na ukatili wa kingono. (Picha:ConductUnmission)