Watoto 17,000 wametenganishwa na wazazi au familia zao Gaza: UNRWA
Watoto 17,000 wametenganishwa na wazazi au familia zao Gaza: UNRWA
Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limeonya hii leo juu ya idadi kubwa ya watoto ambao wako peke yao Gaza, ama wamepoteza wazazo au kutenganishwa nao pamoja na jamaa wa familia wakati huu ambapo hawawezi kuhudhuria masomo na shule nyingi zikigeuka kuwa makazi ya wakimbizi wa ndani.
Kwa mujibu wa tarifa fupi ya UNRWA iliyotolewa kupitia ukurasa wake wa X, shirika hilo linasema maisha ya watoto Gaza yamekuwa jinamizi na takriban 17,000 wako peke yao hawana wazazi au walezi ama wametenganishwa na familia zao.
Pia imesema watoto hao wahaudhurii masomo kutokana na vita inayoendelea kwani zaidi ya asilimia 70 ya nyumba zimesambaratishwa au kubomolewa na watoto wengi wamepoteza nyumba zao.
UNRWA imeongeza kuwa shule sasa zimelazimika kuwa mkazi ya manusura wa vita hivyo na sio mahala pa elimu tena na kufanya mustakbali wa watoto hao kuwa njiapanda na unahitaji kulindwa.
Viatu vya watoto vimetapakaa barabarani
UNRWA inasema viatu vya watoto vinonekana kutelekezwa katika mamia mamia ya mita huko Khan Younis
Picha zinaonyesha viatu vilivyotapakaa chini, vilivyoachwa haraka walipokuwa wakikimbia mashambulizi ya anga au kujaribu kuhama makazi yao, wananchi wengi wa Gaza waliacha makazi yao na kukimbia bila viatu vinavyofaa.
Kwa kukimbia, bila viatu, au picha za viatu hivi vilivyoachwa pia zinaweza kuwa dhihirisho la mashambulizi ya anga katika maeneo fulani ya eneo la Palestina.
Kulingana na Louise Waterridge, afisa wa mawasiliano wa Shirika la UNRWA, "watu walikimbia haraka sana hata viatu waliviacha huko Khan Younis."
Kwenye mtandao wa kijamii wa X UNRWA imeandika “Maelfu ya familia zimekuwa zikihifadhiwa katika shule hizi za UNRWA zilizogeuzwa kuwa makazi kabla ya kushambuliwa. Mambo mengi yameachwa nyuma,” ameeleza Louise Waterridge.
Maelfu ya viatu vinaashiria maisha yaliyopotea Gaza
Ushuhuda huu kutoka kwa afisa wa mawasiliano wa UNRWA unakuja wakati video nyingi, haswa kwenye mitandao ya kijamii, zinaonyesha watoto wakitafuta chakula, wakati mwingine na hali mbaya ya viatu vya raia wa Gaza.
Wakati wengine "wakivuka vifusi, vioo vilivyovunjika na taka zingine ngumu bila viatu", video hizi zinatoa ushuhuda wa maisha ya kila siku ya watoto wa Gaza, pamoja na viatu vimetelekezwa kwenye vichochoro vya eneo la Palestina.
Suala la viatu hivi pia linachukuliwa wakati wa maandamano juu ya vita huko Gaza.
Ripoti za vyombo vya habari zilionyesha kuwa katika baadhi ya miji ya Ufaransa, wanaharakati wakati mwingine waliweka mamia ya viatu vya watoto wakati wa maandamano.
Katika mji mkuu wa Hispania pia, picha za video zilionyesha maelfu ya viatu vimewekwa mbele ya ukumbi wa jiji la Madrid katikati ya mwezi Desemba, kuwakilisha Wapalestina waliouawa huko Gaza tangu Oktoba 7.
Maandamano yanyofanyika nchini Uholanzi, maelfu ya viatu vya watoto pia viliwekwa kwenye Medani ya Vredenburg huko Utrecht ili kuashiria maelfu ya watoto wa Kipalestina waliouawa katika Ukanda wa Gaza katika kipindi cha miezi mitano iliyopita.
Kuendelea kugawa msaada
Ni katika hali hiyo ndipo Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF lilipoendelea na usambazaji wa nguo katika maeneo mbalimbali yakiwemo Rafah, Khan Younis na Deir Al-Balah.
Tangu Oktoba 7, mwaka 2023, UNICEF na washirika wake wamesambaza zaidi ya nguo 203,000 vya nguo zinazofaa kuvaliwa kwa watoto wenye umri wa miaka 0 hadi 17.
Zaidi ya hayo, Louise Waterridge amerejea katika kituo cha mafunzo cha UNRWA huko Khan Younis ambako anasema "kumesalia watu kidogo sana na ambapo zaidi ya watu 40,000 walikuwa wamekimbilia wakati jengo liliposhika moto kutokana na operesheni ya kijeshi ya Israel na ilikuwa imezingirwa. Vyumba vyote vimeungua, vitu vimetawanyika kila mahali.”
Louise Waterridge anesema “Kwenye makaburi ya watoto uani tunaweza kusoma unamkumbuka dada yako.
Kutokana na hali mbayá ya hewa na ongezeko la joto UNRWA inasema watu wengi wanhaha hata kupata mahitaji muhimu kama maji ya kunywa ambapo wakimbizi wa ndani wanapokea chini ya lita moja ya maji kwa mtu kwa ajili ya kunywa, kufua na kuonga ikiwa ni tofauto kubwa na lita 151 ambacho ni kiwango cha chini wanachostahili kupata.
Na jana Jumapili UNRWA na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya msaada w uteguzi wa mabomu UNMAS walianza operesheni muhimu ya kutathimini uharibifu katika vituo vya UNRWA kuweka alama kwa makombora yoyote na vifaa vyovyote ambavyo hvijalipuka.
Mitambo 165 ya UNRWA huko Ukanda wa Gaza imeathiriwa wakati wa vita hii inayoendelea.
Na UNMAS inasema ili kuifanya Gaza kuwa salama dhidi ya vifaa vya milipuko ambayo haijalipuka inaweza kuchukua miaka 14.