Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu wa UN akaribisha makubaliano yaliyofikiwa nchini Ethiopia

Wanawake na watoto wakisubiri msaada wa chakula kwenye eneo la mgao la Adimehamedey huko jimboni Tigray nchini Ethiopia.
© WFP/Claire Nevill
Wanawake na watoto wakisubiri msaada wa chakula kwenye eneo la mgao la Adimehamedey huko jimboni Tigray nchini Ethiopia.

Katibu Mkuu wa UN akaribisha makubaliano yaliyofikiwa nchini Ethiopia

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekaribisha makubaliano yaliyofikiwa jana Novemba 12,2022  kati ya makamanda wakuu wa jeshi la Ethiopia na Kikosi cha Ukombozi cha Watu wa Tigrayan ya kuanzisha mbinu za utekelezaji wa Mkataba wa Kudumu wa Kusimamisha Uhasama (COHA).

Taarifa iliyotolewa leo na Ofisi ya Msemaji wa Katibu Mkuu huyo jijini New York Marekani imeeleza utayari wa Umoja wa Mataifa kuunga mkono mchakato huu muhimu.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Katibu Mkuu Guterres ametoa wito kwa pande husika kusonga mbele na jambo hilo la dharura katika kutafsiri makubaliano haya kuwa maboresho madhubuti kwa ajili ya raia walioko mashinani, ikiwa ni pamoja na kuongeza kasi ya kuwezesha upatikanaji wa misaada ya kibinadamu na kurejesha huduma muhimu.