Tigray

Tunaendelea kusikitishwa na mauaji na machafuko Tigray:OCHA 

Umoja wa Mataifa umesema unaendelea kusikitishwa na kuendelea kwa taarifa za raia kujeruhiwa na kuuawa kwa raia  wakati wa mapigano yanayoendelea katika maeneo ya vijijini jimboni Tigray nchini Ethiopia na kutiwa hofu kubwa kuhusu janga la maelfu ya watu ambao bado hawajapokea msaada kwenye jimbo hilo kwa zaidi ya miezi miwili na nusu sasa tangu kuzuka kwa machafuko jimboni humo. 

Wakimbizi kutoka Ethiopia wanaoingia Sudan, UNHCR yaendelea kuwapokea na kuwaandikisha.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linaendelea kuandikisha wakimbizi wapya katika mpaka wa Sudan na Ethiopia amb

Sauti -
2'2"

UNHCR inaendela kupokea na kuandikisha wakimbizi kutoka Ethiopia wanaoingia Sudan

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linaendelea kuandikisha wakimbizi wapya katika mpaka wa Sudan na Ethiopia ambapo takriban wakimbizi 800 wamevuka kutoka eneo la Tigray nchini Ethiopia na kuingia mashariki mwa Sudan katika siku chache za mwaka huu wa 2021.

29 DESEMBA 2020

Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea

Sauti -
12'22"

Kutoka Tigray na ujauzito hadi kujifungulia ukimbizini Sudan

Kufurushwa kwa maelfu ya raia wa Ethiopia kutokana na mapigano kwenye jimbo la Tigray kumekuwa janga zaidi kwa wajawazito ambao wamejikuta wanalazimika kutembea muda mrefu na kujifungulia ugenini. Miongoni mwao ni Nigsty ambaye anasema matarajio yake ni amani irejee nyumbani ili  yeye na mwanae warejee Salama!
 

Wakimbizi 25,000 kutoka Eritrea wapokea msaada jimboni Tigray Ethiopia:UN

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamefikisha msaada wa chakula wa kuokoa Maisha kwa wakimbizi 25,000 kutoka Eritrea walioko kwenye jimbo la Tigray nchini Ethiopia. 

Uchunguzi ufanyike kuhusu madai ya mauaji ya raia Tigray- Bachelet

Baada ya kuibuka kwa mapigano katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia wiki saba zilizopita, kutofikishwa kwa misaada ya kibinadamu katika eneo hilo pamoja na kukatishwa kwa mawasiliano katika maeneo mengine vinatia wasiwasi hali ya wananchi, ameonya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa mataifa, Michelle Bachelet.

Dola milioni 156 zahitajika kusaidia wanaokimbia ghasia Tigray- UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR pamoja na wadau 30 wa kibinadamu  hii leo wanatoa wito wa dharura kupatiwa wa dola milioni 156.
 

Hofu na taharuki zinazingira safari za wakimbizi kutoka Tigray wakati wakikimbia machafuko

Mzozo wa Ethiopia ukiendelea, familia moja iliyotenganishwa walipokimbia eneo la Tigray la Ethiopia ina bahati ya kuungana tena nchini Sudan, lakini wasiwasi juu ya maisha yao ya baadaye ni mzito.

Sauti -
2'43"