Asilani ukiukwaji wa haki za binadamu usiachwe uwe mazoea:Bachelet 

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet
UN Photo/Antoine Tardy
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet

Asilani ukiukwaji wa haki za binadamu usiachwe uwe mazoea:Bachelet 

Haki za binadamu

Kamishina Mkuu haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo amelaani, hali mbaya inayoendelea kuongezeka duniani ya ukiukwaji mkiubwa wa haki za binadamu wakati wa ufunguzi wa kikao cha 47 cha Baraza la Haki za Binadamu la mjini Geneva Uswis.

Michelle Bachelet amesema "Ni heshima kuhutubia Baraza hili wakati wa maadhimisho ya miaka 15 lakini kwa bahati mbaya hii inaambatana na kipindi cha mapungufu makubwa ya haki za binadamu, umasikini uliokithiri, ukosefu wa usawa na udhalimu unaongezeka. Fursa za kidemokrasia na za kiraia pia zimeendelea kubinywa mfano China, Urusi na Ethiopia. Pia amesema masuala kama umasikini uliokithiri, pengo la usawa na vitendo vya watu kunyimwa haki imekuwa kitu cha kawaida."
Bibi Bachelet anaamini kwamba kizazi cha sasa cha viongozi wa ulimwengu kitalazimika kupata suluhisho la wazi la kujikwamua kutoka kwenye janga la corona au COVID-19 na kuchukua hatua za pamoja kusaidia kujikwamua vyema kutokana na kuzorota vibaya kwa haki za binadamu kuwahi kushuhudiwa. 
Kwa hivyo ni juu ya "kusonga mbele kwa umoja, kiikolojia, kwa uendelevu na mustakbali wenye mnepo la sivyo tutanguka".


Kuendelea kwa ukiukaji wa haki za binadamu Tigray

Watu waliotawanywa na machafuko kwenye jimbo la Tigray Kaskazini mwa Ethiopia
© UNICEF/Zerihun Sewunet
Watu waliotawanywa na machafuko kwenye jimbo la Tigray Kaskazini mwa Ethiopia

Kamisha huyo mkuu amesema anawasiwasi sana juu ya hali katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia, na "habari zinazoendelea zinayoonyesha ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa za kibinadamu na ukiukaji wa hali ya juu wa haki za binadamu na unyanyasaji wa raia kutoka kwa pande zote kwenye mzozo. Kwa hivyo kuongezeka kwa mauaji ya kiholela, watu kukamatwa kiholela na kuwekwa kizuizini, pamoja na unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto na watu wazima”.
Kauli hizi za Bi Bachelet zinakuja wakati ambao uchaguzi wa wabunge unafanyika Jleo Jumatatu nchini Ethiopia. Kwa kuongezea, Bi Bachelet amesema "dalili za kuaminika" zinaonyesha kuwa wanajeshi wa Eritrea bado wapo huko Tigray. 
Vikosi vya Asmara vinaendelea kutekeleza ukiukwaji wa haki za binadamu na ukiukaji wa sheria za kibinadamu za kimataifa, amesema.
Hivi karibuni Umoja wa Mataifa umekadiria kuwa watu 350,000 wako katika hatari ya kufa njaa. 
Kwa Bi Bachelet, hali ya kibinadamu ni "mbaya, huku kukiwa na ripoti za watu kunyimwa fursa za upatikanaji wa misaada ya kibinadamu katika baadhi ya maeneo na uporaji wa vifaa vya misaada unaofanywa na na wanajeshi."
Kwa mujibu wa Kamishina huyo mkuu wasiwasi mwingine, ni mvutano unaongezeka katika nchi nzima. Katika maeneo mengine mengi ya Ethiopia, matukio ya kutisha ya unyanyasaji mbaya wa kikabila na baina ya jamii na makazi yao ukihusishwa na ubaguzi unaokua juu ya malalamiko ya muda mrefu. 
"Upelekaji wa sasa wa vikosi vya jeshi sio suluhisho la kudumu", amesema Bi Bachelet, akitaka "mazungumzo ya kina nambalimbali yanahitajika kote nchini ili kushughulikia malalamiko halisi yanayotolewa."
Wakati huo huo, huduma za Kamishna Mkuu Bachelet na Tume ya Haki za Binadamu ya Ethiopia zitakamilisha uchunguzi wake juu ya ukiukaji wa haki za binadamu kaskazini mwa Ethiopia.

Maelfu ya watu wamefurushwa kutokana na vurugu kaskazini mwa Burkina Faso.
© UNHCR/Moussa Bougma
Maelfu ya watu wamefurushwa kutokana na vurugu kaskazini mwa Burkina Faso.

Kwa kufanyika kwa uchaguzi huru nchini Chad na Mali

Kwa upande wa bara la Afrika, mkuu huyo wa haki za binadamu wa amesema "ana wasiwasi sana na mabadiliko ya hivi karibuni ya kidemokrasia na ya kikatiba ya serikali huko Chad na Mali". 
Mabadiliko ambayo bila shaka yanawakilisha "changamoto kubwa kwa haki za binadamu na ambayo yamedhoofisha ulinzi wa taasisi ya uhuru za kidemokrasia".
Lakini, Bi Bachelet anabainisha kuwa serikali za mpito za nchi hizo mbili zimethibitisha azma yao ya kuheshimu majukumu ya kisheria ya kimataifa, haswa katika eneo la haki za binadamu.
"Naungana na wahusika wengine wa kimataifa kutoa wito wa kuimarishwa vita dhidi ya kutokujali, kwa michakato ya mpito ya kidemokrasia inayoshiriki kikamilifu, ikiwa ni pamoja na kufanyika kwa uchaguzi huru na wa haki, na kurudi haraka na kikamilifu kwa utaratibu wa kikatiba katika nchi za Chad na Mali” ameongeza.