Ustadi na jitihada za sungura viwe chachu tunapokabili magumu ya dunia, asema Guterres katika salamu za mwaka mpya wa kichina
Chun Jie Kuai Le! Heri ya mwaka mpya wa kichina. Ndio ilivyoanza video ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye ametuma salamu za heri ya mwaka mpya kwa wachina wote ulimwenguni ambao mwaka huu alama yake ni sungura!