Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Adhabu ya kifo haipunguzi idadi ya mauaji: Bachelet

Tukio la hali ya juu kuhusu,hukumu ya kifo.
UN Photo.
Tukio la hali ya juu kuhusu,hukumu ya kifo.

Adhabu ya kifo haipunguzi idadi ya mauaji: Bachelet

Haki za binadamu

Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema hakuna ushahidi kwamba adhabu ya kifo itakuwa na matokeo mazuri ya kupunguza vitendo vya mauaji.

Bi. Michele Bachelet ameyasema hayo katika mjadala kwenye Baraza la Haki za Binadamu unaoendelea mjini Geneva Uswisi ambapo leo ulijikita na haki ya mtu aliye hukumiwa kifo.

Kamishina huyo amesema “Kinyume chake mataifa ambayo yamefuta hukumu ya kifo yanashuhudia kupungua au utulivu katika masuala ya uhalifu na takwimu hizi zinapaswa kuwa na nguvu kuliko mawazo.”

Rais huyo wa zamani wa Chile amesema ni uhakika wa idhini na sio uzito wa idhini ndio unaowazuia wahusika wa uhalifu huo.

Ameongeza kuwa ushahidi na hoja za kisiasa zinaunga mkono kukomeshwa kwa adhabu ya kifo kila mahali na katika kila hali. Chini ya mazingira haya adhabu hii haina nafasi katika karne ya 21.

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet
UN News/Daniel Johnson
Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet

Ongezeko la mauaji katika baadhi ya nchi zenye hukumu ya kifo 

Kamishina mkuu amesisitiza kwamba “adhabu ya kifo ni kinytume na utu wa binadamu na inamnyima mtu haki za msingi, kwanza kabisa haki ya kuishi”

Akiunga mkono tathimini ya Bi Bachelet, mjumbe wa kamati ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa , Christopher Arif Bulkan amebainisha kuwa nchi ambazo zimesalia na adhabu ya kifo na zinaendelea kuitekeleza zinashindwa kupunguza viwango vyao vya mauaji.

“Hivyo ndivyo ilivyo mathalani katika baadhi ya nchi za Carinnea ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Madola. Licha ya kuwepo kwa adhabu ya kifo kiwango cha mauji kinaongezerka kila mwaka n ahata kusalia kuwa miongoni mwa nchi zenye viwango vya juu vya mauaji duniani mfano Trinidad na Tobago”.

Bwana Bulkan ameongeza kuwa hii ni njia moja wapo ya kudhihirisha ushahidi uliopo kwamba hukumu ya kifo haizai matunda kama chachu ya kukomesha uhalifu.

Ni katika mazingira ya kipee kabisa na yenye ushahidi usiopingika ndipo sheria za kimataifa zinaruhusu adhabu ya kifo (Kutoka Maktaba)
©UNICEF/Josh Estey
Ni katika mazingira ya kipee kabisa na yenye ushahidi usiopingika ndipo sheria za kimataifa zinaruhusu adhabu ya kifo (Kutoka Maktaba)

Kuna mifano mingi inayojulikana kimataifa ambayo inaunga mkono madai haya ikiwemo Canada, Ulaya Mashariki, na hata Marekani ambako kukomesha na kubadili hukumu za kifo kumeleta tija ya kupunguza kiwango cha mauaji kwa kiasi kikubwa.

Chad ilifuta hukumu ya kifo Aprili 2020

Mtaalam huyo wa kamati ya haki za binadamu anashikilia kwamba hata kuna kiwango cha juu cha jeuri kwa njia ambayo adhabu hiyo inatumika.

Kuna mambo mengi yasiyo na maana kwenye adhabu ya kifo.

Na mtaalam huyo huru wa Umoja wa Mataifa anasema adhabu ya kifo inatumika kwa walio hatari zaidi na makosa yanaweza na yanatokea.

“Kushikilia adhabu ya kifo kuna mtazamo kama ni ishara bora lakini ukweli ni kwamba si jawabu bora au zuri kwa uhalifu na machafuko.”

Akitolea mfano Chad mtaalam huyo amesema imerejea kwenye barabara ndegfu ambayo imeipelekea kukomesha hukumu ya kifo na ilikuwa ni mwaka 2017 ambapo kwenye makao makuu ya nchi hiyo D’Djamena kanuni za adhabu na utaratibu wa makosa ya jinai zilirekebishwa ili kuzingatia sheria za kimataifa. 

Kukomeshwa kwa adhabu ya kifo kuliamriwa kwa makosa ya kawaida ya kisheria isipokuwa vitendo vya kigaidi ambavyo viliendelea kuhukumiwa na sheria yam waka 2015.

Lakini mwaka janda 2020 serikali ya Chad ilipitisha sheria ya kufuta vitendo vote vya kigaidi na kufuta maandishi ya sheria ya zamani ya 2015.

Na tangu wakati huo, Chad imekomesha kabisa hukumu hiyo na imelichukua taifa hilo miaka 50 kufikia hatua hiyo.

Na leo hii kutokomeza adhabu ya kifo ni moja ya hatua mujarabu za marekebisho ya sheria na utekelezahi wa haki za binadamu nchini Chad.