Kama wazalishaji wakubwa wa chanjo tutahakikisha ya COVID-19 inamfikia kila mtu:India 

27 Septemba 2020

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi Jumamosi Septemba 26 ameihakikishia jumuiya ya kimataifa kwamba nchi yake ikiwa ni miongoni mwa wazlishaji wakubwa wa chanjo duniani, uwezo wake wa kuzalisha na kusambaza chanjo utatumika ili kusaidia binadamu wote kupambana na janga la corona au COVID-19. 

Katika hotuba yake kwa njia ya video kwenye mjadala wa Batraza Kuu la Umoja wa Mataifa waziri mkuu Modi amesema “Hata wakati huu mgumu wa janga la corona sekta ya madawa ya India imepeleka dawa muhimu kwa nchi zaidi ya 150 duniani.” 

Ameongeza kuwa “Nchini India na majirani zetu tunasonga mbele na awamu ya tatu ya majaribio inayofanyika India. India pia itazisaidia nchi zote kuimarisha uwezo wa kuhifadhi na kutunza dawa hizo kwa ajili ya kuzisambaza chanjo.” 

Hotuba ya waziri mkuu huyo kama zilivyokuwa nyingi mwaka huu ilirekodiwa kwa video na kuchezwa kwenye ukumbi wa Baraza Kuu mjini New York Marekani . 

Licha ya kushindwa kuwaleta viongozi wa dunia kukusanyika New York mjadala wa mwaka huu utashuhudia ushiriki mkubwa zaidi wa wakuu wan chi na serikali katika historia ya Umoja wa Mataifa. 

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter