Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuko tayari kurejea kwenye ulingo wa kimataifa, lakini tunahitaji msaada:Sudan

Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Adam Hamdok pichani akihutubia mjadala wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGAS75
UN Photo/Manuel Elías
Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Adam Hamdok pichani akihutubia mjadala wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGAS75

Tuko tayari kurejea kwenye ulingo wa kimataifa, lakini tunahitaji msaada:Sudan

Masuala ya UM

Waziri mkuu wa Sudan Abdalla Adam Hamdok ameuambia mjadala wa Baraza Kuu leo Jumamosi kwamba taifa lake liko tayari kuchangioa tena katika jumuiya ya kimataifa lakini litahitaji msaada wakati likijitahidi kufufu uchumi wake iliosambaratika. 

Hivi sasa taifa hilo la Afrika linaendelea na mwelekeo wa mpito wa kisiasa baada ya kuenguliwa kwa Rais Omar al-Bashir mwezi Aprili mwaka 2019. 

Waziri mkuu huyo amesemaSudan na damu ya wanamapinduzi imepitia miongo ya changamoto, kutokuwepo haki na kuzorota kwa hali ya kijamii. Lakini licha ya yote haya kipindi hili cha mpito cha mapinduzi ya vijana kinakabiliwa na changamoto nyiongi pia ambazo zinahitaji msaada wa jumuiya ya kimataifa ili kuweza kuendesha mipango na miradi ya serikali ambayo inalenga kuboresha hali ya uchumi.” 

Kudorora kwa uchumi 

Waziri mkuu Hamdok ametoa ombi hilo katika hotuba yake ya kwanza kwa Baraza Kuu iliyorekodiwa kwa njia ya video na kurushwa moja kwa moja ndani ya ukumbi wa Baraza hilo mjini New York. 

Wakuu wa nchi na serikali wanashiriki katika mjadala wa mwaka huu kwa njia ya mtandao kwa sababu ya janga la corona au COVID-19 

Bwana. Hamdok amesema serikali ya mpito ya Sudan imerithi uchumi uliosambaratika na dhaifu, sekta za huduma zilizoathirika ikiwemo mfumo wa afya ambao umetelekezwa kwa miongo kadhaa. 

Ameongeza kuwa “na adui wa giza janga la COVID-19 limeongeza zahma . Sudan pia imekumbwa na mvua kubwa zilizosababisha mafuriko ambayo yameleta athari mbaya ikiwemo ku[poteza Maisha ya wat una mali. Maerlfu kwa maefu ya nyumba ama zimesambaratishwa kabisa au zimebomolewa kiasi.” 

Mipango ya kusaidia familia 

Mamlaka hiyo mpya ya Sudan inafanya mabadiliko ili kujenga upoya uchumi na waziri Hamdok ameelezea mipango ya baadaye ambayo inajumuisha kutoa msaada wa kijamii kwa familia masikini na kuimarisha uzalishaji wa kilimo kote mijini na maeneo ya vijijini. 

Tunafanya juhudi zetu zote kuzitathimini sheria zetu za kitaiofa na kuhakikisha kwamba zinakwenda sanjari na mikataba na kanuni za kimataifa “. 

Waziti mkuu Hamdok alikuwa anazungumzia juhudi za kusafisha sheria za sasa za uhuru wa kujieleza, za ulinzi wa haki za wanawake na ukwepaji sheria miongoni mwa mambo mengine. 

Hata hivyo waziri mkuu ameeleza kwamba msaada wa kimataifa ni muhimu endapo wanataka kuhakikisha mabadiliko ya kiuchumi yatafanyika. 

Kwa mantiki hiyo kusamehewa madeni na fursa za kipekee ni suala la kipaumbele. 

Sudan pia inapaswa kuondolewa katika orodha ya nchi ambazo zinafadhili magaidi ameongeza waziri mkuu huyo. 

“Sudan imerejea katika ulingo wa kimataifa baada ya miaka 30 kuwa nje. Hili lazima litimie lakini tunahitaji msaada na kuungwa mkono ili kufanikisha hilo. Ni matumaini yetu kwamba tunaweza kutimiza miradi ya ujenzi mpya na mabadiliko ili Sudan iwe kwa mara nyingine iwe mshiriki kiungo katika uwanja wa kikanda na kuchangia katika jumuiya ya kimataifa na kufanya kazi ya kujenga mustakbali tunaoutaka.”