Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COVID-19 inatupa fursa na wajibu wa kuimarisha uhusiano wetu na asili: Guterres

Samaki wa Trevally katika visiwa vya Solomon.
Coral Reef Image Bank/Tracey Jen
Samaki wa Trevally katika visiwa vya Solomon.

COVID-19 inatupa fursa na wajibu wa kuimarisha uhusiano wetu na asili: Guterres

Tabianchi na mazingira

Ikiwa leo ni siku ya bahari duniani , Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema janga la virusi vya Corona au COVID-19 ni kumbusho kwamba binadamu wote wanahusiana wenyewe lakini pia na asili.

Guterres ameyasema hayo kupitia ujumbe wake maalum wa siku hii ambayo kila mwaka huadhimishwa June 8 na kusistiza kwamba wakati dunia ikijitahidi kukomesha janga hili la COVID-19 na kujijenga upya ni fursa muhimu ya kubadilika

“Tuna fursa ya kipekee katika kizazi hiki na wajibu wa kurekebisha uhusiano wetu na ulimwengu wa asili ikiwemo bahari za dunia hii. Tunazitegemea bahari kwa chakula, maisha, usafiri na biashara”

Katibu mkuu ameongeza kuwa wakati mapafu ya dunia hii na kiwango chake kikubwa cha hewa ukaa vikididimia, bahari ina jukumu muhimu sana katika kukabili mabadiliko ya tabianchi lakini

“Leo hii kina cha bahari kinaongezeka kutokana na mabadiliko ya tabianchi na kutishia uhai na maisha katika mataifa madogo na miji ya mwambao na jamii kote duniani. Tindikali inaongezeka baharini na kuweka bayoanuwai ya bahari na mnyororo muhimu wa chakula hatarini.”

Muongo wa sayansi ya bahari

Akuzungumzia pia hilo katika taarifa yake kwenye mkutano maalum wa siku ya bahari unaofanyika kwa njia ya mtandao, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Tijjani Muhammad Bande amesisitiza kwamba matumizi yasiyo endelevu ya rasilimali hii muhimu ya bahari yanatishia uwezo wa bahari kutupa bidhaa muhimu.

Wakati tukiutarajia muongo huo ambao utaanza mwakani namchagiza kila mtu kuchukua hatua haraka kwa kuweka mikakati ya ulinzi ili kuwezesha bahari kuunda dunia bora nchi kavu na baharini kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Maisha chini ya bahari

Mazingira bora yay a viumbe vya baharini ya ufunguo muhimu kwa ajiliya kutimiza ajenda ya malengo ya maendeleo endelevu.

Mwezi Januari muongo wa hatua na utekelezaji ulifunguliwa kutekeleza maendeleo endelevu SDG’s “Ulinzi wa bayoanuwai ya bahari ni muhimu wakati tukipiga hatua za utekelezaji wa SDG14” amesema Bwana Bande na kuongeza kwamba “Katika siku ya bahari ni lazima tuchukue wakati kukumbuka na kushukuru kwa yale yote ambayo bahari zimetutendea . Pia ni fursa kwetu kuganga yajayo hivyo kila mtu anapaswa kuzingatia na kukumbatia umuhimu wa uchumi wa kijani unaojali mazingira na bahari endelevu.”

Ameongeza kuwa uwekezaji wa kimkakati unaweza kuunda ajira milioni 100 ifikapo 2050 na kusaidia katika kujikwamua muhimu duniani baada ya janga la virusi vya corona.

Amesisitiza kwamba “Mwaka huu lazima tuchukue hatua kuzuia tani zingine milioni 8 za taka za plastiki kuingia baharini na kulinda mfumo wa Maisha duniani.”

Bwana Bande amehitimisha kwa kuwataka nchi wanachama wote “Kuahidi kulinda asilimia 30 ya bahari zetu ifikapo 2030 ili kuhakikisha angalau asilimia 30 ya bahari inakuwa miongoni mwa maeneo yaliyolindwa. Hatuwezi kusimama na kuona bahari zikizidi kuwa na tindikali, vina vya maji vikiongezeka na uchafuzi ukiongezeka.”

Kobe ambaye anaozea chini ya bahari akiwa amezingirwa na nyavu na ndoano za uvuvi
UN World Oceans Day/Shane Gross
Kobe ambaye anaozea chini ya bahari akiwa amezingirwa na nyavu na ndoano za uvuvi

Kana kwamba hayo hayatoshi Guterres amesema, uchfuzi utokakanao na taka za plastiki umetapakaa kila mahali.Mwaka huu siku ya bahari imejikita katika ubunifu kwa ajili ya maendeleo endelevu, na Katibu Mkuu anasisitiza kwamba uelewa mzuri wa bahari ni muhimu kwa ajili ya kuhifadhi akiba ya samaki na kubaini bidhaa mpya na madawa.

Kwa mantiki hiyo amesema muongo wa Umoja wa Mataifa wa sayansi ya bahari kwa ajili ya maendeleo endelevu unaokuja hivi karibuni utatoa taswira ya mkakati wa pamoja wa kuchukua hatua kwa ajili ya bahari.

Hivyo amezitaka serikali na wadau wote kuahidi na kujikita na uhifadhi na uendelevu wa bahari kupitia ubunifu na sayansi.