Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yatoa ombi la dola bilioni 6.7 kulinda mamilioni ya watu dhidi ya COVID-19 katika nchi masikini

Binti mdogo katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Khair Al-Sham Syria
© OCHA
Binti mdogo katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Khair Al-Sham Syria

UN yatoa ombi la dola bilioni 6.7 kulinda mamilioni ya watu dhidi ya COVID-19 katika nchi masikini

Msaada wa Kibinadamu

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA ametoa wito wa kuchukuliwa hatua Madhubuti ili kuepuka athari kubwa za mlipuko wa janga la corona au COVID-19 wakati akitoa ombi la dola bilioni 6.7 huku akieleza mipango ya kimataifa ya kupambana na virusi vya corona katika nchi zisizojiweza.

Mkuu huyo Mark Lowcock, amesema hivi sasa COVID-19 imefika katika kila nchi , kukiwa na karibu wagonjwa milioni 3,596,000 waliothibitishwa na vifo Zaidi ya 247,650 kote duniani.

Hali katika nchi masikini

Bwana Lowcock ameongeza kuwa “kilele cha ugonjwa huo katika nchi masikini kabisa bado haakijafika na kinatarajiwa Zaidi ya miezi mitatu hadi sita ijayo. Hata hivyo amesema tayari kuna Ushahidi kipato kuporomoka na ajira kutoweka , minyororo ya usafirishaji wa chakula nayo imeathirika na bei kupanda na pia watoto wakikosa likizo na vyakula.”

Amesisitiza kwamba hivi sasa mfumo wa masuala ya kibinadamu unachukua hatua ili kuepuka kuongezeka kwa vita, njaa, umasikini na magonjwa kutokana na janga hili na mdororo wa kiuchumi unaoikumba dunia hivi sasa.

Mpango mpya wa kimataifa wa masuala ya kibinadamu uliotangazwa leo umepanua wigo wa msaada wake na sasa kujumuisha nchi nyingine zisizojiweza na kuwa katika hali hatarishi zikiwemo Benini, Djibout, Liberia, Msumbiji, Pakistan, Ufilipino, Sierra Leone, Togo na Zimbabwe ambapo mipango pia inahusisha hatua za kukabiliana na ongezekoo la kutokuwa na uhakika wa chakula.

Mkuu wa shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP Achim Steiner na mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA, Mark Lowcock, wakizungumza na wakulima mji wa mpakani wa Banki jimboni Borno, Nigeria.
@OCHA/Eve Sabbagh
Mkuu wa shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP Achim Steiner na mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA, Mark Lowcock, wakizungumza na wakulima mji wa mpakani wa Banki jimboni Borno, Nigeria.

Ombi la leo la fedha

Ombi la leo la fedha na pia mipango mipya ya msaada wa kibinadamu limezinduliwa kwenye mkutani uliofanyika kwa njia ya mtandao mwenyeji akiwa mkuu wa OCHa Mark Lowcock , akishirikiana na mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP David Brasley, mkurugenzi wa shirika la afya duniani WHO wa kitengo cha dharura za kiafya Mike Ryan, Rais wa Oxifarm Marekani Abby Maximan, na Kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCr Filippo Grandi. Mpango huo ulizinduliwa mara ya kwanza mwezi Machin a Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Umuhimu wa ombi la leo

Akizungumzia umuhimu wa ombi la leo mkuu wa OCHA Mark Lowcock amesema “Janga la COVID-19 linatuumiza sote lakini athari kubwa na mbaya zitakuwa katika nchi masikini kabisa duniani. Katika nchi masikini tayari tunashuhudia uchumi ukisinyaa kutokana na kushuka kwa mapato ya kusafirisha nje bidhaa, kupungua kwa kiwango cha fedha zinazotomwa toka nje na kutoweka kwa utalii. Tusipochukua hatua sasa lazima tujiandae kw ongezeko kubwa la migogoro, njaa na umasikini. Hali ya baa la njaa inanyemelea.”

Shirika la Umoja wa  Mataifa la mgao wa chakula WFP wakipeana chakula kwa familia za Aleppo, Syria na kuhakikisha wanajikinga kutokana na Virusi vya Corona.
WFP/Khudr Alissa
Shirika la Umoja wa Mataifa la mgao wa chakula WFP wakipeana chakula kwa familia za Aleppo, Syria na kuhakikisha wanajikinga kutokana na Virusi vya Corona.

Amesisitiza kwamba endapo hatutawasaidia masikini hususan wanawake na wasichana na makundi mengine yaliyo katika hatari wakati huu yakipambana na janga la corona na athari za mdororo wa kimataifa wa uchumi , basi tutakabiliwa na athari mbaya za kuzishughulikia kwa miaka mingi ijayo ambazo zitadhihirika kuwa za mauamivu makali zaidi na za gharama kubwa zaidi kwa kila mtu.

Mkpango wa kimataifa wa kushughulikia janga la COVID-19 ni nyezno ya jumuiya ya kimataifa ya kuchangisha fedha ili kukabiliana na athari za virusi vya corona katika nchi za kipato cha kati na cha chini na kusaidia juhudi zao za kupambana na janga hilo.

Mpango huo unaleta pamoja maombi ya WHO na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kibinadamu. Mashirika yasiyo ya kiserikali yaani NGOs na vyama vya NGOs yamekuwa chahu kubwa katika kuunda mpango huo, ni wadau wakubwa katika kuhakikisha fedha zinapatikana na fedha zinaweza kufikiwa kupitia wao.

Mpango huo unatoa msaada na ulinzi ambao unaweka kipaumbele kwa walio katika hatari Zaidi. Haw ani pamoja na wazee, watu wenye ulemavu na wanawake na wasichana, ukizingatia kwamba jnga la COVID-19 limezidisha kiwango cha ubaguzi uliokuwepo, pengo la usawa na ukatili wa kijinsia. Pia mpango unajumuisha hatua za kukabiliana na ongezeko la kutokuwepo na uhakika wa chakula.

Mkuu wa WHO

Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus akitoa taarifa kuhusu mlipuko wa COVID-19 mjini Geneva
UN Photo/Eskinder Debebe)
Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus akitoa taarifa kuhusu mlipuko wa COVID-19 mjini Geneva

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus amesema “idadi ya wagonjwa katika nchi nyingi zilizojumuishwa kwenye mpango wa usaidizi wa kibinadamu inaweza kuwa ndogo lakini tunajua kwamba uwezo wa ufuatiliaji, upimaji maabara na mifumo ya afya katika nchi hizi ni dhaifu.Hivyo kuna uwezekano mkubwa kwamba kuma maambukizi yanayoendelea kwenye jamii ambayo bado hayajabainika.”

Pia ameongeza kwamba wakati huohuo hatua zingine za kuzuia watu kusalia majumbani na nyinginezo za kuepuka maambukizi zina athari kubwa katika huduma muhimu za afya. Hivyo amesema ni muhimu sana kuhakikisha huduma hizi kuanzia chanjo, hadi huduma za afya ya uzazi, huduma za usafi (WASH) na huduma za afya ya akili.

Mkuu wa shirika la wakimbizi UNHCR

Kamishna Mkuu wa wakimbizi kwenye Umoja wa Mataifa Filippo Grandi akiwalaki wakimbizi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, waliorejea nyumbani kutoka DRC.
© UNHCR/Adrienne Surprenant
Kamishna Mkuu wa wakimbizi kwenye Umoja wa Mataifa Filippo Grandi akiwalaki wakimbizi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, waliorejea nyumbani kutoka DRC.

Filippo Grandi, kamishina mkuu wa wakimbizi akipaza sauti yake katika ombi hilo amesema “janga hili linaacha vidonda vikubwa kote duniani , kwa watu ambao walikimbia vita na mateso athari za mlo na kipato chao cha kila siku na kwa jamii zinazowahifadhi zimekuwa kubwa sana. Kwa kushirikiana na wadau wetu NGO, Umoja wa Mataifa umedhamiria kuhakikisha tunawasaidia wakimbizi, wakimbizi wa ndani, watu wasio na utaifa na jamii zinazowahifadhi, na kuhakikisha kwamba wanajumuisha katika hatua za afya za umma na hifadhi ya jamii.”

Pia amesisitiza kwamba mahitaji yao ni makubwa lakini sio ya kiwango cha kutosaidika, n ani kwa hatua za pamoja tu ndio dunia itaweza kulishinda tishio hili la janga la corona na kuokoa maisha.”Hatua ambazo ni za wakati, za kujitolea na za aina mbalimbali kutoka kwa washirika wetu wote ni muhimu sana”

Mkurugenzi mtendaji wa WFP

David Beasley,mkuu wa mpango wa chakula duniani, akizuru Sanaa, Yemen amabko mgorgoro mkubwa wa njaa umekuwa ukiendelea kwa mwaka sasa.
WFP/Marco Frattini
David Beasley,mkuu wa mpango wa chakula duniani, akizuru Sanaa, Yemen amabko mgorgoro mkubwa wa njaa umekuwa ukiendelea kwa mwaka sasa.

Naye mkurugenzi mtendaji wa WFP David Brasly akisisitiza umuhimu wa shikamano katika ombi la leo amesema “ Katika siku yoyote WFP inatoa msaada wa kuokoa Maisha kwa karibu watu milioni 100, endapo tutashindwa kuendele na operesheni hizo muhimu basi janga hili la kiafya muda si mrefu litageuka janga la njaa ni muhimu kwa jumuiya ya kimataifa kutimiza hatua hizi za kibinadamu na kuweka mfumo imara wa mipango ambayo itawalinda raia walio katika hatari zaidi dhidi ya majanga ya kibinadamu.”

Tangu mpango huo ulipozinduliwa 25 Machi mwaka huu dola bilioni 1 imeshangawa kutoka kwa wahisani. Fedha hizo zinajumuisha dola milioni 166 kutoka mfuko wa OCHA za kusaidia nchi 37, dola milioni 95 kutoka mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF na dola milioni 12 kutoka mifuko ya usaidizi katika nchi 12.