15 FEBRUARI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia kazi za Umoja wa Mataifa kwa waathirika wa tetemeko la ardhi, na pia kazi za umoja huo nchini Ukraine. Makala tunakupeleka nchini Burundi na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?
Hii leo jaridani tunaangazia kazi za Umoja wa Mataifa kwa waathirika wa tetemeko la ardhi, na pia kazi za umoja huo nchini Ukraine. Makala tunakupeleka nchini Burundi na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?
Hii leo jaridani tunaangazia wanawake na wasichana katika sayansi, na msaada wa binadamu mashariki ya kati kwa waathirika wa tetemeko la ardhi. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Misri, kulikoni?
Hii leo jaridani tunakwenda mashariki ya kati na nchini Ukraine. Makala tutaelekea nchini Tanzania na mashinani tutasikia ujembe wa mchehemuzi wa vijana wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na pia mwanasayansi.
Hii leo jaridani tunaangazi siku ya kimataifa ya kutokomeza ukeketaji wa wanawake na wasichana, FGM na kazi za UNICEF nchini Yemen.
Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina ambapo leo tunakwenda nchini Kenya kumulika harakati za elimu ikiwa ni kuelekea siku ya elimu duniani. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo kutoka IAEA, msaada wa kibinadamu nchini DRC na matokeo ya mkutano wa Baraza la Usalama wa Umoja wa Mataifa. Mashinani tunakwenda nchini Uganda. Katika kujifunza kiswahili tunapata ufafanuzi wa msemo "FUNGA FUNGANYA"
Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina tukimulika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mkataba wa kimataifa wa bayoanuai CBD unaoendelea mjini Montreal Canada. Pia tunakuletea habari kwa ufupi kutoka huko huko Montreal Canada, nchini Somalia na nchini Haiti. Mashinani tunakuletea ujumbe wa mwanauchumi mashuhuri duniani Sir Partha Dasgupta, anasemaje?
Charlotte Fatuma na Neema Cenga ni wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na sasa wanaishi ukimbizini nchini Msumbiji katika jimbo la Nampula. Kwa sasa Charlotte ni mjasiriamali mwenye mafanikio makubwa, akiendesha biashara ya duka kwenye makazi ya wakimbizi ya Coranne huku Neema naye akijitahidi kulea na kusomesha watoto wake.
Hii leo katika Habari za UN tunamulika msaada wa kibinadamu, tabianchi, mafuriko Nigeria na hakarati za kukabili mmomonyoko wa udongo Kenya.
Hii leo katika Habari za UN Assumpta Massoi anamulika masuala yafuatayo:
1. Ukame uliolighubika eneo la Pembe ya Afrika kwa miongo minne mfululizo umesababisha changamoto kubwa kwa mamilioni ya raia wa hilo ikiwemo Kenya, Ethiopia na zaidi Somalia ambako maeneo mengi yanakabiliwa na kutokuwa na uhakika wa chakula na hatihati ya kutumbukia kwenye baa la njaa. Mashirika ya misaada ya kibinadamu likiwepo la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP yako msitari wa mbele kuwasaidia watu wenye uhitaji hususani wa chakula.
Vita nchini Ukraine inaendelea kuathiri huduma katika sekta ya afya pamoja na minyororo ya ugavi ambayo mamia ya maelfu ya watu wanaoishi na ukimwi na walioathiriwa na virusi vya ukimwi, VVU wanategemea kuishi.