Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanafunzi Tanzania kujifunza kupitia redio na televisheni kutokana na COVID-19

Wanafunzi kutoka shule ya msingi ya Minyinyi, nchini Tanzania na mwalimu wao ambaye anawafundisha kutumia kifaa cha kupima rutuba kwenye ardhi kwa ajili ya vipimo vya mbolea.
FAO Tanzania

Utamaduni na Elimu

Nchini Tanzania, wito wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO, wa kuhakikisha wanafunzi wanaendelea kujifunza hata wakati wa huu wa kusalia majumbani kutokana na janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19, umeanza kutekelezwa ambapo hii leo Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imezindua rasmi urushaji wa vipindi vya masomo kupitia televisheni na Radio.

Uzinduzi huo umefanywa kwenye mji mkuu wa Tanzania Dodoma na Katibu Mkuu wa  Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo ambapo amesema. "Vipindi hivi ni vya masomo mbalimbali kwa ngazi ya elimu ya awali,elimu ya msingi na elimu ya kutoka Kidato cha  cha kwanza mpaka cha sita,vipindi hivi vitasambazwa katika vyombo mbalimbali vya habari huku nchini ili masomo yaweze kufikia wanafunzi wetu nchi nzima. Lengo kubwa la kutoa vipindi hivi ni kuwaezesha wanafunzi waendelee kujifunza wakati huu ambapo wako nyumbani,katika kipindi hiki ambapo shule zao zimefungwa."

Madarasa yako wazi lakini elimu inaendelezwa kwa kutumia teknolojia wakati huu wa kukabiliana na COVID-19
CC0 Public Domain
Madarasa yako wazi lakini elimu inaendelezwa kwa kutumia teknolojia wakati huu wa kukabiliana na COVID-19

Dkt.Akwilapo amesema wizara yake iliandaa vipindi hivyo kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania. Lakini vipi kuhusu lugha? "Hata hivyo urushwaji wa vipindi hivi hauna maana ya kuwa mbadala wa masomo ya darasani mara baada ya shule hizi kufunguliwa baada ya janga hili kuwa limekwisha. Kwa hivyo tunawasihi walimu wataendelea na mitaala yao kama inavyoelekezwa kwenye taratibu zetu za kila siku sio kwamba wataruka mambo ambayo yatakuwa yamerushwa kwenye vipindi hivi."

Akaenda mbali zaidi kuzungumzia wanafunzi wa kidato cha sita waliokuwa wafanya mitihani.

"Baraza la mitihani la Tanzania limeandaa vipindi  kwa ajili ya maandalizi ya watahiniwa wa kidato cha sita nayo pia yatarushwa kwenye vyombo hivi.Vipindi hivi vitawawezesha watahiniwa hawa kufanya marudio ya mada mbalimbali amdazo wataalam wa baraza la mitihani wameona ni vizuri zikafanyiwe marejeo  nadhani walikuwa wanaangalia mada ambazo zinakuwa na maswali magumu wakati wa kufanya mtihani."

Katibu Mkuu huyo amesema vipindi hivyo havitakuwa mbadala pindi shule zitakapofunguliwa na kwamba walimu wataendelea kufundisha kwa kufuata mitaala hata kama kuna matangazo ya radio na televisheni.