Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maendeleo ya kielimu wakati wa COVID-19 yanahitajii utashi wa kisiasa na ushirikiano wa kila upande. 

Watoto darasani Sakassou, Côte d'Ivoire.(8 Julai 2019)
© UNICEF/Frank Dejo
Watoto darasani Sakassou, Côte d'Ivoire.(8 Julai 2019)

Maendeleo ya kielimu wakati wa COVID-19 yanahitajii utashi wa kisiasa na ushirikiano wa kila upande. 

Utamaduni na Elimu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, kwa njia video ameuambia mkutano wa ngazi za juu ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kuwa kazi ya kudumisha ujifunzaji wa wanafunzi wakati wa janga la COVID-19 haitoshi na akasihi kuwe na utashi wa kisiasa kuzuia mamilioni ya watoto na vijana barubaru kupoteza haki yao ya kupata elimu.

Mkutano huo wa kimataifa kuhusu elimu ambao unafanyika mjini Paris Ufaransa, umewahusisha wakuu 11 wa mataifa na serikali, pia Mawaziri 62 wa elimu, maafisa wa Umoja wa Mataifa na Balozi Mwema wa Umoja wa Mataifa kupitia shirika la kuhudumia wakimbizi, muigizaji Angelina Jolie.  

“Tangu mwanzo wa janga la coronavirus">COVID-19, takribani theluthi moja ya wanafunzi ulimwenguni wamenyimwa aina fulani ya masomo. Kufungwa kwa shule kwa sasa kunaathiri wanafunzi wapatao milioni 500. Kundi lililotengwa zaidi takribani wasichana milioni 11 lina hatari kubwa ya kutorudi tena shuleni.” Ameeleza  Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa katika mkutano huo uliofadhiliwa na serikali za Ghana, Norway na Uingereza pamoja na  Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO.  

Bwana Guterres ameonesha kuwa taarifa iliyoidhinishwa wakati wa mkutano huo, kulingana na ripoti yake ya sera aliyoitoa kwa ajili ya elimu na pia rasmu au waraka uliowasilishwa leo, inaonesha nia ya wahudhuriaji kutokomeza "athari hizi hasi na kuepuka janga la kizazi kizima." 

Hata hivyo Katibu Mkuu Guterres, aamefafanua kuwa kufanya nyaraka au tamko waliloidhinisha kuwa kitu halisi itategemea zaidi mambo matatu: utashi wa kisiasa, uvumbuzi na ushirikiano mzuri wa pande zote. 

Uwekezaji mkubwa katika elimu 

Katika tamko hilo, ambalo linajumuisha wakuu wa nchi na serikali; mawaziri na wajumbe; na wawakilishi wa mashirika ya UN, mashirika ya kimataifa na ya kikanda, asasi za kiraia na waalimu, miongoni mwa watendaji wengine katika sekta hiyo, imekubaliwa kudumisha kujitolea kwa Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu, hasa lengo namba 4 lililoelekezwa kwa elimu bora. 

Kwa kuongezea, ili kupunguza athari za COVD-19, kwa makadirio ya kufikia dola bilioni 200 kila mwaka katika nchi zenye kipato cha chini na cha chini kati ikiwa hatua hazitachukuliwa na ushirikiano wa ulimwengu katika elimu kuimraishwa, imekubaliwa kuwekeza kwa haraka katika elimu bora iliyo jumuishi, yenye usawa na kuelimika wakati wote.  

Angelina Jolie: Elimu haiwezi kuwekwa mateka na uchumi 

Muigizaji Angelina Jolie kutoka California Marekani amewaambia wadau wa elimu na viongozi duniani kwamba kuna haja ya kuwahusisha vijana katika mijadala ya namna hii na akisisitiza kuwa haipaswi kuwa watoto wanaotoka tu katika nchi salama na zilizo imara bali watoto  ambao wako katika mazingira yasiyo bora. 

Pia ameonesha haja ya kuwa na fedha za kutosha kwa sababu "hatuwezi kuzungumzia juu ya kulinda elimu bila kuitetea", na akaonyesha kwamba licha ya shinikizo za kiuchumi ambazo nchi zinateseka, "kujaribu kusawazisha mizani kwa gharama ya elimu itakuwa kujiharibu na kimaadili huwezi kuitetea hali hiyo.”