Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwaka 2010-2013

Kutoka kushoto: Malala Yousafzai anahudhuria hafla ya elimu katika Makao makuu ya UN; Watu watembea katika barabara za Port-au-Prince kufuatia tetemeko la ardhi la mwaka 2010 huko Haiti; Mlinda amani wa UN kwenye doria huko Kidal, Mali
UN Photo.

Masuala ya UM

Muongo huu ulianza kwa simanzi ya janga kubwa nchini Haiti, ambapo tetemeko la ardhi la ukubwa wa  7.0 vipimo vya richa mnamo Januari 12 mwaka 2010.

Kufuatia tetemeko hilo nusu ya mji mkuu Port-au-Prince ulisambaratishwa, watu 220,000 walipoteza maisha na wengine milioni 1 kuachwa bila makazi.

Haiti imepitia misiba ya asili kwa muda wa miaka 15 hadi sasa. Hapa, mlinda amani wa UN kutoka Brazili amebeba mtoto ambaye aliokolewa kufuatia mafuriko katika kitongoji cha Cité Soleil cha Port-au-Prince.
UN Photo/Marco Dormino
Haiti imepitia misiba ya asili kwa muda wa miaka 15 hadi sasa. Hapa, mlinda amani wa UN kutoka Brazili amebeba mtoto ambaye aliokolewa kufuatia mafuriko katika kitongoji cha Cité Soleil cha Port-au-Prince.

Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa waliokuwa Haiti waliathirika pia na 102 kati yao akiwemo mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Hédi Annabi pamoja na naibu wake Luiz Carlos da Costa walipoteza maisha.

Katika kuwaenzi wafanyakazi wake waliopoteza maisha Umoja wa Mataifa uliahidi kuendelea na kazi zake na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati huo Ban Ki moon alisema

(SAUTI YA BAN)

“walibeba mwanga wa matumaini, kamwe hatutowasahu tutaendeleza kazi zenu.”

Mwaka 2011 ulishuhudia pia matukio mengi ambayo athari zake zinaendelea kuonekana mpaka sasa, mfano maandamano yaliyojulikana kama wimbi la maandamano Mashariki ya kati yaliyoambatana na machafuko na vifo vingi . Mwezi Oktoba Muammar Al-Gaddafi aliyekuwa kiongozi wa Libya wakati huo aliuwawa.

Miaka minane baadaye mzozo wa Syria bado unaendelea huku mamia ya maelfu ya watu wamefariki dunia , zaidi ya watu milioni 5.6 wamekimbia mwako na wengine milioni 6.6 ni wakimbizi wa ndani kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.

Familia zinazokimbia machafuko kaskazini mashariki mwa Syria wakiwasili Tal Tamar, wakiwa ni vitu vidogo ambazo wameweza kubeba wakati wakikimbia machafuko.
© UNICEF/Delil Souleimain
Familia zinazokimbia machafuko kaskazini mashariki mwa Syria wakiwasili Tal Tamar, wakiwa ni vitu vidogo ambazo wameweza kubeba wakati wakikimbia machafuko.

Mwaka huo huo wa 2011 mwezi Julai, nchi changa kabisa duniani Sudan Kusini ilizaliwa baada ya kupata uhuru kutoka kwa Sudan na kuwa mwanachama wa 193 wa Umoja wa Mataifa.

Somalia nayo ilikumbwa na ukame mkubwa kuwahi kushuhudiwa watu milioni 1.5 wakilazimika kukimbia makwao kuelekea nchi jirani ikiwemo Kenya  kwenye kambi ya wakimbizi ya Dadaab na wengi walipoteza maisha wakiwa safarini.

Mfugaji kaskazini mwa Somalia katika jimbo lililokumbwa na ukame, alipoteza takribani nusu ya kondoo wake ambao walikuwa wamefikia 70.
Photo: UNICEF/Sebastian Rich
Mfugaji kaskazini mwa Somalia katika jimbo lililokumbwa na ukame, alipoteza takribani nusu ya kondoo wake ambao walikuwa wamefikia 70.

Mwaka 2012  ni mwaka ambao, kijana barubaru Malala Yousafzai kutoka Pakistan alipigwa risasi na kundi la Taliban  mwezi Oktoba wakati akichukua basi kuelekea nyumbani kutoka shule  alinusurika kifo. Tukio hilo liligonga vichwa vya Habari kote ulimwenguni na kulaaniwa vikali pia lilimfanya kuwa barubaru maarufu kwa muongo huo na hata kuenziwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO na baadaye tuzo ya amani ya Nobel.

Naibu Katibu Mkuu wa UN Amina J. Mohammed (kushoto) akizungumza na Malala Yousafzai, mchechemuzi wa haki ya elimu kwa watoto wa kike na pia mshindi mwenye umri mdogo zaidi wa tuzo ya amani  ya Nobel.
UN / Evan Schneider
Naibu Katibu Mkuu wa UN Amina J. Mohammed (kushoto) akizungumza na Malala Yousafzai, mchechemuzi wa haki ya elimu kwa watoto wa kike na pia mshindi mwenye umri mdogo zaidi wa tuzo ya amani ya Nobel.

Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo endelevu ulifanyika katika mji mkuu wa Brazil, Rio de Janeiro.

Mabango ya maendeleo endelevu kama yanavyoonekana katika viwanja vya Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani Septemba 20,2019
UN News/Conor Lennon
Mabango ya maendeleo endelevu kama yanavyoonekana katika viwanja vya Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani Septemba 20,2019

Lakini pia sehemu ya jeshi ilipindua serikali na mapigano kuzuka Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC kati ya vikosi vya serikali na waasi yalipelekea watu milioni 2 kukimbia makwao na kuwaacha watoto milioni moja hatarini.

Mnamo Aprili mwaka 2013 ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu Mali, MINUSMA  ulianzishwa , wati Congo DRC mapigano mapya yalifurusha watu laki moja kutoka makwao jimbo la Kivu  na Baraza la Usalama kwa mara ya kwanza lilipitisha azimio la kuruhusu kikosi cha kujibu mashambulizi ADF kukabiliana waasi wa M23.

Walinda amani kutoka ujumbe wa  Umoja wa Mataifa nchini Mali, MINUSMA wakiwa kwenye kikao cha haki na maridhiano kwenye jimbo la kati la Mopti nchini humo
MINUSMA/Gema Cortes
Walinda amani kutoka ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, MINUSMA wakiwa kwenye kikao cha haki na maridhiano kwenye jimbo la kati la Mopti nchini humo

Nchini Somalia mwaka 2013 baada ya kipindi cha miaka 20 ya vurugu na miaka miwili tangu kufurushwa kwa kundi la Alshabab rais wa kwanza achaguliwa kidemokrasia.

Na mwa huu pia kwa mara ya kwanza siku ya choo duniani iliadhimishwa  Novemba 19 katika kuikumbusha dunia kwamba mabilioni ya watu wanaishi bila choo.