Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutambua taaluma za wakimbizi kutawasaidia kuanza upya maisha katika nchi zinazowahifadhi:UNESCO

Wanawake katika jimbo la Copperbelt nchini Zambia wanaofanya kazi katika mfumo wa kilimo bora wanaongeza uzalishaji wa mbogamboga wanaouza katika masoko ya wenyeji( kutoka maktaba 2015)
ILO/Marcel Crozet
Wanawake katika jimbo la Copperbelt nchini Zambia wanaofanya kazi katika mfumo wa kilimo bora wanaongeza uzalishaji wa mbogamboga wanaouza katika masoko ya wenyeji( kutoka maktaba 2015)

Kutambua taaluma za wakimbizi kutawasaidia kuanza upya maisha katika nchi zinazowahifadhi:UNESCO

Wahamiaji na Wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na wadau wengine wameendesha tathimini ya kwanza kabisa ya usaili wa taaluma kwa wakimbizi kwenye makazi ya wakimbizi ya Maheba nchini Zambia. 

Kwenye makazi ya wakimbizi ya Maheba jimbo la Kaskazini Magharibi mwa Zambia wahamiaji na wakimbizi kutoka nchi mbalimbali wanaoishi hapa wamekusanyika kwenda kukutana na maafisa wa UNESCO, UNHCR na wasaili wa masuala ya taaluma kutoka shirika la Norway la uhakiki wa ubora na mamlaka ya taaluma ya Zambia kwa ajili ya kufanyiwa usaili  wa taaluma zao. 

Hii ni mara ya kwanza kabisa UNESCO kuendesha zoezi hili ambapo wahamiaji na wakimbizi wanatahiniwa ili kubaini taaluma zao kwani wengi walipoteza vyeti vyao vya awali na hapa wanapatiwa Veti vipya vya pasi mpya za kutambulisha taaluma zao baada ya usaihili. Timothee Yanda Tshilumbu ni mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC , ni daktari

(SAUTI YA TIMOTHEE TSHULUMBU)

“Nimeridhishwa na usahili, nimefurahi na nimeguswa sana kwa sababu itatupatia fursa ya kupata paspoti ya UNESCO ya taaluma. Na ninataka kuweka bayana kwamba pasi hii sio ya kusafiria ila ni nyaraka ambayo inatambua kiwango chako cha elimu au kitu gani ulichosomea, hivyo itawezesha elimu yetu kutambuliwa"

UNESCO inaamini kwamba paspoti hii ya kutambua kiwango cha elimu kilichotokana na usaili itachangia kwa kiasi kikubwa kwa wahamiaji na wakimbizi kuanza Maisha mapya katika nchi zinazowahifadhi. Castrol Singelengele ni afisa wa wakimbizi kutoka wizara ya ndani ya Zambia anayehudumu kwenye makazi ya Maheba.

(SAUTI YA CASTROL SINGELENGELE)

“Nadhani Paspoti hii ya taaluma ni nyaraka muhimu sana, ni nyenzo muhimu kwa ajili ya wakimbizi wakati huu, hususan kile walichokuwa wanakikosa hapo awali ni nyenzo hii ambayo itawawezesha kupata kazi au kuingia shule kueweza kuendeleaza elimu yao. Kwa hivyo kimsingi naamini huu utakuwa uwezeshaji mkubwa kwa wakimbizi na hsa kwa kuchagiza ujumuishwaji wao”

Naye Catherine Atata Walumba mkimbizi toka DRC ambaye ana stashahada ya ualimu baada ya kusailiwa na kufuzu kupata fursa sasa ya kuendeleza elimu yake anatoa wito kwa wakimbizi wengine kwenye makazi hayo

(SAUTI YA CATHERINE ATATA)

“Nawachagiza wapate elimu, kwa sababu elimu ni ufunguo wa mafanikio".

UNESCO na wadau wake wamesema huo ni mwanzo tu na  wameahidi kurejea tena kuendesha zoezi lingine kama hilo.