Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua tulizopiga miaka 25 iliyopita hazitoshi, mamilioni ya wanawake na wasichana wanasalia nyuma- Bi. Mohammed

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed akihutubia maadhimisho ya 25 ya ICPD mjini Nairobi Kenya
UNFPA
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed akihutubia maadhimisho ya 25 ya ICPD mjini Nairobi Kenya

Hatua tulizopiga miaka 25 iliyopita hazitoshi, mamilioni ya wanawake na wasichana wanasalia nyuma- Bi. Mohammed

Afya

Hatua iliyopigwa kwa miaka 25 tangu kupitishwa azimio la kihistoria la Cairo 1994 la hatua za kumkomboa mwanamke na mtoto wa kike bado mchakato ni tete na mamilioni wanaachwa nyuma amesema naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini Nairobi Kenya.  

Akizungunmza hii leo mjini Nairobi Kenya katika maadhimisho ya 25 tangu kupitishwa azimio hilo la Cairo Bi. Amina J. Mohammed amesema “mtazamo wa azimio hilo ulikuwa na bado uko bayana kuwawezesha wanawake na wasichana kupata haki zao ili waweze kudai uhuru wao, afya na ustawi wao kwa ajili ya faida za muda mrefu za familia zao, jamii zao na mataifa yao.”

Amesema licha ya hatua kubwa zilizopigwa kutokana na kujitolea na kazi iliyofanywa katika shughuli na kampeni mbalimbali  cha kusikitisha wakati tukitathimini hayo cha kusikitisha  ni kwamba mchakato huu ni tete na mamilioni ya wanawake na wasicha unawaacha nyuma. Hivyo amesema“Tunahitaji kuongeza hatua haraka kutekeleza mpango wa hatua wa azimio hilo ili kutimiza malengo ya maendeleo endelevu. Hili ni muhimu wakati tukiingia katika muongo wa hatua za kufanikisha SDGs.”

Amesisitiza kwamba dunia bado ni ngumu na mara nyingi ni mahali pa hatari kwa mamilioni ya wanawake na wasichana. Na ili kufanya isiwe ngumu zaidi ,viongozi katika maeneo yote wanahitaji kuboresha utekelezaji wa ahadi za Cairo, za kupata mustakabali mzuri kwa vijana wetu haswa wasichana wetu. Na kwamba“kama wachagizaji wa malengo ya maendeleo endelevu , matokeo ya mpango huu wa kuchukua hatua ni lazima uendelezwe. Mkakati wetu wa pamoja kwa ajili ya watu , kwa ajili ya sayari yetu , ustawi , amani na ushirika vinategemea hilo”

Ameongeza kuwa mustakabali endelevu utawezekana tu endapo ahadi iliyowekwa kwa mamilioni ya wanawake na wasichana miaka 25 iliyopita itatimizwa.

Hivyo amesema, "nategemea kila mmoja wenu na kwa pamoja kutimiza ahadi, kulinda mustakabali wa wasichana wetu na kuwawezesha wanawake."

Changamoto zinazowakabili wanawake

Bi. Mohammed amesema kila siku inawakilisha janga kwa wanawake na wasichana ambao wanakufa waliketa uhai mwingine duniani, kwa wasichana wanaolshinikizwa kuingia katika ndoa za utotoni, kwa wasichana ambao sehemu zao za siri zinakatwa na kwa karibu mwanamke1 kati ya 5 au wasichana ambao wanafanyika ukatili au kupoteza maisha yao katika mikono ya wenzi wao ay watu wa familia zao kila mwaka.

Ameongeza kuwa inasikitisha kwamba wanawake milioni 5 wajawazito wanaotawanywa na machafuko  au majanga wanahitaji huduma za afya , na kwamba wanawake wengine milioni 232 hawawezi kuzuia mimba kwa sababu hawana fursa za kupata dawa za uzazi wa mpango wanazohitaji na haki ya kuzipata.

Mkutano huu amesema naibu Katibu Mkuu ni fursa ya kipekee kusaidia kuwainua wanawake na wasichana , familia zao na jamii zao na kujenga dunia bora yenye haki na chaguo kwa wote. “ Katika zama hizo za ukuaji wa miji , ongezeko la uhamiaji, ongezeko la idadi ya watu na ungezoko la wazee , mkakati wa kuchukua hatua unamaana na muhimu kuliko wakati mwingine wowote.”

Hivyo amesema tunahitaji haraka kukusanya nguvu za kisiasa na kasi ya kifedha ili kusongesha mbele ajenda ya ICPD hususan katika pengo lililopo baina ya nchi , kupunguza idadi ya vivyo vya kina mama wakati wa kujifungua na vifo vya watoto wachanga na kumaliza matatizo ya dawa za uzazi wa mpango , lakini pia kukomesha ukatili na vitendo vya kikatili dhidi ya wanawake na wasichana.

Amelipongeza shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA akisema kupitia mikakati na miaradi yake mbalimbali limeongeza fursa za huduma za afya ya uzazi , katika kupunguza na kukabiliana na ukatili wa kijinsia, kupambana na ukeketaji kwa wanawake na wasichana, ndoa za utotoni na kuwawezesha vijana.

Nini kifanyike

Amesema pamoja na jitihada hizo tunahitaji kuratibu msaada na hatua kwenye mfumo mzima wa Umoja wa Mataifa  wa maendeleo ili kutimiza ahadi ya ICPD ili kuweza kushuhudia kukomeshwa kwa ndoa za utotoni na ukeketaji kwa wasichana. Tunaweza kutimiza hili na takwimu zinaonyesha hivyo.