Mashirika ya UN yashikamana kukabili changamoto za miji:UN-HABITAT

30 Mei 2019

Umoja wa Mataifa umesema changamoto za miji zinahitaji mshikamano sio tu wa Umoja wa Mataifa na mashirika yake bali wa kimataifa ili kuweza kufikia ajenda ya 2030 ya amendeleo endelevu yaani SDGs.

Katika baraza la shirika la makazi la Umoja wa Mataifa UN-HABITAT litakalokunja jamvi hapo kesho Mei 31zaidi ya washiriki 3000 wamekusanyika wakiwemo mawaziri, magavana, mameya, wakuu wa makampuni ya biashara na asasi za kiraia yakiwemo pia mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa ili kusaka suluhu mujarabu ya changamoto zinazoikamili miji duniani.

UN photo/Jean Marc Ferré
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed

Leo kupitia ujumbe maalum wa video uliopewa jina “Mazungumzo ya UN moja” kwenye mkutano huo naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed, amesisitiza kuwa “Kushughulikia mwenendo wa ukuaji wa miji ili kuchagiza maendeleo endelevu kutahitaji mtazamo wa mfumo mzima na hatua za pamoja katika ngazi zote.”

Ameongeza kuwa katika miaka miwili iliyopita Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekuwa akifanya mabadiliko ili kuhakikisha kwamba mfumo wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa unaweza kusaidia utimizaji wa malengo 17 ya maendeleo ikiwemo ajenda ya miji.

Wadau wengine

Ili kuonyesha mshikamano wao viongozi mbalimbali wa ofisi na mashirika ya Umoja wa Mataifa wamezungumza kwenye baraza hilo kuhusu umuhimu wa kufanya kazi pamoja kutimiza ajenda ya maendeleo ya miji.

© 2019/ Julius Mwelu/UN-Habitat
Waziri Mkuu wa Yemen, Dr. Moeen Abdul Malik Saeed akikaribishwa na mkurugenzi mtendaji wa UN-Habitat pemebeni ni kaimu Mkurugenzi Mkuu wa UNEP, Joyce Msuya.

 

Joyce Msuya, kaimu mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP amesema mwelekeo ni mchakato mpya wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya SDGs uliopitisha mapema mwezi huu wa Mei 2019 ambao utauwezesha Umoja wa Mataifa kuboresha takwimu za miji na nyenzo za kutathimini kwa usawa na athari za ukuaji wa miji katika ukuaji wa uchumi, mabadiliko ya tabianchi na hatua za kuzuia na kupambana na majanga.

“Ushirikiano utakuwa nguzo muhimu kuyafanikisha yote haya, ni lazima tuutumie vyma mchango wa asasi za kiraia, sekta binafsi, wanazuoni, jamii na wengine wanaoweza kuchangia.”

Mkakati wa mfumo mzima wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya SDGs ulianzishwa kwa mchakato wa ushirikiano baina ya uongozi wa mashirika 42 ya Umoja wa Mataifa pamoja na uongozi wa shirika la Fedha Duniani IMF na Benki ya Dunia.

 

Julius Mwelu/ UN Habitat
Mkurugenzi mtendaji wa UN-HABITAT Maimunah Mohd Sharif akihutubia baraza la shirika la makazi la Umoja wa Mataifa UN-HABITAT jijini Nairobi Kenya.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendahji wa UN-HABITAT Maimunah Mohd Sharif amekumbushia vipaumbele vya Umoja wa Mataifa katika suala la ukuaji wa miji kama moja ya mienendo inayoendelea kuongezeka na kutambua kwamba ukuaji wa miji ni suala muhimu kwenye kufikjia malengo ya maendeleo endelevu au SDGs.

 “Ili kuchagiza ushirika muhimu katika mfumo mzima wa Umoja wa Mataifa makakati umeainisha mambo manne ya msingi Mosi: usawa na kutokomeza umasikini, Pili:mafanikio na ukuaji wa uchumi, tatu:hatua za mabadiliko ya tabianchi na ulinzi wa mazingira na nne:kukabiliana na majanga na kuyazuia na mambo haya manne ndio yawe dira ya kazi yetu.”

Akiongezea hapo Joyce Msuya amesema jinsi tutakavyodhibiti miji yetu ndiko kutakakotuwezesha kufanikiwa katika SDGs. Miundombinu ikihitajika kujengwa kwa asilimia 70 ifikapo mwaka 2050 tuna fursa muhimu ya kuinyakua kwa kupanga maendeleo ya miji katika mfumo bora zaidi.

 

@UN-HABITAT
Waziri mkuu wa Fiji Josai Vorege Bainimarama (Katikati) akilakiwa na Mkurugenzi mtendaji wa UN-HABITAT Maimunah Mohd Sharif (Kushoto)na rais wa Baraza la UN-Habitat Martha Delgado (kulia) wakiwasili kwenye mazungumzo ya baraza hilo Nairobi Kenya

Naye Rais wa Baraza la UN-HABITAT Martha Delgado, amesema anaona mmkakati wa mfumo mzima wa umoja wa Mataifa kwa ajili ya SDGs ni fursa kwa ajili ya ushirikiano.

 “Kuna haja ya kupanga njia bora Zaidi ya kuwaleta pamoja watu wote wa Umoja wa Mataifa ili Umoja wa Mataifa usiwe umefunkwa kwa watu. Hatuka kitu lilichokaribu kwa watu kama serikali zao za mashinani na za kitaifa.

 

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud