ICPD25

10 Julai 2020

Hii leo Ijumaa ni mada kwa kina tunakwenda Dodoma nchini Tanzania kuona jinsi Restless Development wamesaidia kuinua uelewa wa vijana kuhusu afya ya uzazi, kuelekea siku ya watu duniain kesho Julai 11, 2020 inayomulika miaka 25 tangu azimio la Cairo. Neno la wiki leo kwenye kujifunza Kiswahili tunaye Aida Mutenyo kutoka Uganda na methali Enga kabla ya Kujenga, lakini pia kuna habari ya ufupi kubwa zaidi ni Bosnia na Herzegovina. Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu.

Sauti
11'58"
UNFPA

Vijana tutumie fursa ili kufanikisha azimio la Cairo kuhudu idadi ya watu na maendeleo- Restless Development

Mwaka 1994 huko mjini Cairo Misri kulifanyika mkutano wa kimataifa kuhusu idadi ya watu na maendeleo, ICPD ambao uliibuka na azimio lenye mambo makuu manne, ambayo ni elimu kwa wote ifikapo mwaka 2015, kupunguza vifo vya watoto wachanga na watoto, kupunguza vifo vya wajawazito na kuhakikisha kuwa huduma za afya ya uzazi ikiwemo uzazi wa mpango zinapatikana kwa watu wote ikiwemo vijana wa kike na wa kiume.

Sauti
3'52"
UN Photo/Laura Jarriel

Mafanikio ya azimio la Cairo kuhusu watu na maendeleo yatasalia finyu bila ushiriki wa vijana- Restless Development

Mkutano wa maadhimisho ya 25 ya azimio la ICPD ukiendelea mjini Nairobi Kenya imeelezwa kuwa mchango wa vijana ni muhimu sana katika utekelezaji wake na kuhakikisha kwamba hakuna mwanamke na msichana anayesalia nyuma katika ejenda ya maendeleo endelevu.

Kauli hiyo inaungwa mkono pia na washiriki mbalimbali wa mkutano akiwemo Sima Bateyunga mshiriki kutoka shirika lisilo la kiserikali la Restless Development nchini Tanzania ambalo linajikita na masuala ya vijana. 

Sauti
1'19"
UNFPA/Georgina Goodwin

Tutimize kile tulichokubaliana Cairo mwaka 1994- Dkt. Kanem

Miaka 25 ilityopita dunia iliweka ahadi ya kuhakikisha afya ya uzazi kwa wanawake na wasicha inakuwa ni haki ya msingi ili kuwawezesha kuwa huru na kufanya maamuzi ya maisha yao. Sasa umewadia wakati wa kutimiza ahadi hiyo kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa shirika la idadi ya watu duniani UNFPA, Dkt. Natalia Kanem. Priscila Lecomte na ripoti kamili.

Sauti
2'40"
UNZimbabwe/2018

Kuelekea ICPD 25, Zimbabwe yachukua hatua madhubuti kunusuru vifo vya wanawake na watoto wa kike

Miaka 25 iliyopita huko Cairo Misri nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa waliazimia kupunguza na hatimaye kutokomeza vifo vya wanawake, wajawazito, watoto wachanga na watoto ili hatimaye dunia hii iwe na ustawi kwa wote bila kujali mtu anaishi eneo gani. Mataifa yalichukua hatua kwa kuzingatia kuwepo kwa mazingira hatarishi si tu kwa mama mjamzito na mtoto anayejifungua bali pia mila potofu na mazingira yanayomuozesha mapema mtoto wa kike na kumnyima haki ya kupata huduma za uzazi wa mpango. Sasa mataifa ikiwemo Zimbabwe yamechukua hatua, je yamefanya nini?

Sauti
3'30"