Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka 25 iliyopita dunia iliweka ahadi sasa ni wakati wa kuitimiza:ICPD 25 

Mtoa huduma azungumza kuhusu afya ya uzazi na wanaume na wanawake.
Diana Nambatya/Photoshare
Mtoa huduma azungumza kuhusu afya ya uzazi na wanaume na wanawake.

Miaka 25 iliyopita dunia iliweka ahadi sasa ni wakati wa kuitimiza:ICPD 25 

Afya

Miaka 25 ilityopita dunia iliweka ahadi ya kuhakikisha afya ya uzazi kwa wanawake na wasicha inakuwa ni haki ya msingi ili kuwawezesha kuwa huru na kufanya maamuzi ya maisha yao. Sasa umewadia wakati wa kutimiza ahadi hiyo kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa shirika la idadi ya watu duniani UNFPA, Dkt. Natalia Kanem.

Dkt. Kanem ameyasema hayo katika mkutano wa maadhimisho ya miaka 25 ya azimio la ahadi hiyo ya ICPD mjini Nairobi Kenya na kumbusha kwamba , miaka 25 iliyopita dunia ilikuwa mahali tofauti sana, simu ya rununu ilikuwa inaenea ndani ya mkomba, lakini leo hii dunia nzima inaenea katika simu ya rununu.

Pia amesema miaka hiyo 25 iliyopita watu walikuwa wanaendesha magari, leo hii magari yanaweza kuendesha watu. Wakati huo wanasayansi walianza kuweka data za viasili nasaba na sasa unaweza kubaini kiasili nasaba chako mwenyewe.

Dkt. Kanem amesisitiza kuwa kuna hatua kubwa zilizopigwa katika maeneo mengi lakini anahoji “Kwa nini hatushuhudii hatua hizo kubwa katika amasuala ya afya ya wanawake na haki zao, wakati miaka 25 iliyopita viongozi wa dunia walikubaliana kuwa afya ya uzazi na haki ni kipaumbele cha dunia?.

Uzazi wa mpango
UNFPA
Uzazi wa mpango

Amesema viongozi hao walito wito wa upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi kote duniani. Nafis Sadik kutoka UNFPA alikuwa katibu mkuu wa mkutano huo miaka 25 iliyopita

“Familia zenye afya bora zinaundwa kwa chaguo na sio kwa kubahatisha”

UNFPA inasema hata hivyo leo hii zaidi ya wanawake milioni 200, bado hawawezi kupata huduma za kisasa za uzazi wa mpango ingawa vifo vya kina mama wakati wa kujifungua vimepungua kwa asilimia 40.

Hata hivyo amesema wito wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake ni changamoto kwani leo hii bado mwanamke mmoja kati ya watatu anapitia ukatili wa kijinsia katika maisha yake.

Viongozi waliweka ahadi miaka 25 iliyopita na Dkt. Kanem anasisitiza sasa ni wakati wa kuitimiza kwa vitendo

“Wanawake na wasichana wamesubiri vya kutosha , umewadia wakati sisi wote kuongeza kasi”

Mkutano huo wa kimataifa wa ICPD 25 umewaleta pamoja zaidi ya washiriki 6,000 wakiwemo viongozi wa dunia, wanazuoni, wanaharakati, viongozi wa kidini na wadau wengine kwa lengo moja, la kutoa wito wa kuchukua hatua kutokomeza vifo vya kina mama wakati wa kujifungua, ukatili wa kijinsia na kukidhi mahitaji ya uzazi wa mpango ndani ya miaka 10. Mkutano huo utakunja jamvi Novemba 14.