Dunia imetokomeza virusi vya polio aina ya 3, huu ni ushindi mkubwa - WHO/UNICEF

24 Oktoba 2019

Katika kuadhimisha siku ya polio duniani hii leo Oktoba 24 shirika la afya duniani, WHO,  limetangaza mafanikio ya kihistoria ya kutokomeza virus ivya polio aina ya 3 au WPV3 duniani kote.

WHO imesema mafanikio haya ya kihistoria yaliyotangazwa na tume huru ya wataalam yamefikiwa duniani kote kufuatia kutokomezwa kwanza kwa ndui na virusi vya polio aina ya 2 na kufanya kuwa ushindi mkubwa katika historia ya binadamu.

Wakizungumzia mafanikio hayo Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt.Tedros Adhamon Ghebreyesus na mwenyekiti wa bodi ya mradi wa kimataifa wa kutokomeza polio (GPEI) wamesema “mafanikio ya kutokomeza polio yatakuwa ni hatua kubwa kwa afya ya kimataifa , ahadi na uwajibikaji kutoka kwa washirika likiwemo shirika laUmoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na nchi,kuongezea na ubunifu vinamaanisha katika aina tatu za virusi vya polio , sasa imebakia aina moja tu. Bado tunasalia katika ahadi na juhudi zetu ili kuhakikisha rasilimali zinazohitajika zipo ili kuweza kutokomeza aina zote za polio. Tunawataka wdau wote na washirika wetu kusalia pia katika vita hivi mpaka mafanikio ya mwisho yatakapopatikana.”

Ugonjwa wa polio una aina tatu ,aina ya 1(WPV1), ya 2(WPV2)  na ya 3 (WPV3), dalili zake zinafanana hasa kwa kusababisha kupooza kutoweza kutibika au vifo, lakini kuna kipengee cha kurithi ambacho hufanya aina zote hizi tatu ni lazima zitokemezwe tofauti.

 

 

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter