Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kusambaa kwa Polio kimataifa bado ni tatizo la afya ulimwenguni-WHO

Mfanyakazi wa UNICEF akitumia kalamu kuweka alama kwenye kidole cha Ajeda Mallam, mtoto wa miezi sita baada ya tu ya kumchanja
UNICEF/Andrew Esiebo
Mfanyakazi wa UNICEF akitumia kalamu kuweka alama kwenye kidole cha Ajeda Mallam, mtoto wa miezi sita baada ya tu ya kumchanja

Kusambaa kwa Polio kimataifa bado ni tatizo la afya ulimwenguni-WHO

Afya

Kusambaa kwa ugonjwa wa polio ambao husababisha kupooza kwa viungo, bado ni tatizo la kimataifa. Maoni hayo yametolewa katika taarifa ilitolewa leo kufuatia mkutano huo wa kamati ya dharura ulioitishwa mjini Geneva Uswisi na shirika la afya duniani, WHO, mkutano ambao unatoa ushauri kwenye masuala ya dharura ya afya ya jamii.

Ni hali ambayo inatokea katika mazingira ambayo ulimwengu ulikaribia kujinasibu kuwa umetokomeza ugonjwa huo unaoishambulia viungo vya binadamu na kusababisha ulemavu usiotibika alkini ambao unaweza kukikgwa kwa kutumia chanjo.

“Kamati, imerekubaliana kuwa hatari ya kusambaa kwa virusi vya polio inasalia kuwa dharura ya kiafya kwa jamii ya kimataifa, PHEIC.” Imefafanua taarifa hiyo ya WHO.

Kamati ya dharura ya WHO imesema ina wasiwasi kuhusu ongezeko la idadi ya visa vya  maambukizi ya polio ya aina ya kwanza (WPV1: kutoka 28 kwa mwaka 2018 hadi 113 kwa mwaka 2019.

“Hali katika nchi ya Pakistan na Afghanstan inaleta wasiwasi.” Ripoti hiyo imeeleza ikifafanua zaidi kwamba, “kwa uwepo wa angalau mtu mmoja aliyeambukizwa duniani, hatari inatishia watoto wote katika sayari.” 

Kamati ikifafanua kuhusu hali ya nchi hizo mbili yaani Pakistan na Afghanistan, imesema kwa kuangalia mwenendo wa virusi, kumekuwa na usambaaji wa virusi kimataifa kutoka Pakistan kwenda Afghanstan na pia kutoka Afghanstan kwenda Paktsan. Kamati imekaribisha hatua ya kuwapatia chanjo watu wa rika zote ambayo inafanyika hivi sasa katika kati ya nchi hizo mbili.

Nchini Nigeria hakujakuwa na visa vyovyote vya polio ya aina ya kwanza yaani WPV1 kwa kipindi cha miaka mitatu na kwa hivyo kuna uwezekano ukanda huo wa Afrika unaweza kutangazwa katika mwaka huu kuwa usio na polio. Kamati imepongeza pia juhudi kubwa za kuwafikia watoto ambao wako katika maeneo magumu kuyafikia huko Borno Nigeria hata katika mazingira ambayo hayana usalama.

Kwa nchi ya Nigeria, kisa cha hivi karibuni cha WPV1 kilichoifanya kuwa katika macho ya dunia kwa ukanda wa Afrika ni kisa cha tarehe 27 mwezi Septemba mwaka 2016.