Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kimbunga Hagibis kikiacha uharibifu mkubwa, UN yaiongeza Japan kwa mnepo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
TASS/ UN DPI
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres

Kimbunga Hagibis kikiacha uharibifu mkubwa, UN yaiongeza Japan kwa mnepo

Tabianchi na mazingira

Wakati kimbunga Hagibis kilichotokana na upepo na mvua kubwa za Typhoon  na kusababisha uharibifu mkubwa na kupotea kwa maisha ya watu nchini Japan, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameipongeza Japan kwa kuwa na mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Katika taarifa iliyotolewa leo Jumapilina msemaji wake Antonio Guterres amesema uongozi wa Japan umechukua jukumu kubwa la kujenga mneno dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na hususan katika maandalizi ya kina dhidi ya tukio hili kubwa la hali ya hewa.


Nalo shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO limekielezea kimbunga hicho Hagibis kuwa ni moja ya vimbunga vilivyokuwa na athari kubwa kuwahi kuikumba Japan katika miaka mingi, kikiambatana upepo mkali, mvua kubwa katika historia, uharibifu wa hali ya juu na mafuriko makubwa nchi kavu na katika maeneo ya pwani.


Kimbunga Hagibis kilitua jana Jumamosi Kusini mwa mji mkuu Tokyo kabla ya kabla ya kuelekea eneo la Kaskazini. Kimbunga hicho kimesababisha uharibifu mkubwa na hasara katika miji yenye watu wengi, kwenye miundombinu na kusababisha takriban vifo 25 na watu wengine 15 hawajulikani waliko.


Vifo hivyo vinasadikiwa ni kutokana na maporomoko ya udongo yaliyoletwa na kimbunga hicho au watu kusombwa na mafuriko.


Kwa mujibu wa duru za habari maelfu ya vikosi vya jeshi, wafanyakazi wa zimamoto na wahudumu wengine wa dharura wamepelekwa katika maeneo yaliyoathirika zaidi ili kuwaokoa watu waliokwama katika mafuriko.


Hadi kufikialeo Jumapili WMO inasema kasi ya kimbunga hicho imepungua na kimeondoka nchi kavu. Makampuni ya huduma za msingi za jamii yamearifiwa yakihaha kujaribu kurejesha nishati ya umeme kwa maelfu na maelfu ya nyumba.


Kimbunga Hagibis kimeikumba Japan mwei mmoja tu baada ya kimbunga Faxai ambacho pia kilisababisha uharibifu mkubwa ukiwemo wa majengo na maelfu ya nyumba ambazo hadi sasa bado hazijakarabatiwa.


Katibu Mkuu katika taarifa yake amesema amestushwa sana na taarifa za vifi vya wat una uharibifu mkubwa ulioachwa na kimbunga Hagibis.


Guterres ametoa pole kwa familia zote za waathirika, serikali na watu wote wa Japan na huku akiwatakia ahuweni ya haraka wote waliojeruhiwa katika zahma hii.