Kuna mwanga wa matumaini Maziwa Makuu licha ya changamoto zilizopo:Xia
Kuna mwanga wa matumaini Maziwa Makuu licha ya changamoto zilizopo:Xia
Eneo la Maziwa Makuu barani Afrika licha ya kuendelea kukabiliwa na changamoto lukuki , kuna mwanga wa matumaini na kupunguza madhila kwa watu wa eneo hilo amesema leo mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika kanda hiyo.
Huang Xia ameyasema hayo kwenye mkutano kuhusu hali ya Maziwa Makuu uliofanyika kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani na pia kuwakilisha ripoti ya Katibu Mkuu ya utekelezaji wa mfumo wa amani, usalama na ushirikiano kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na eneo zima la Maziwa Makuu.
Bwa. Xia amesema ana matumaini na matarajio makubwa kwa eneo la Maziwa Makuu kuliko wakati mwingine wowote kwani eneo hilo hivi sasa limeazimia kuhakikisha amani na utulivu vinarejea. Ameongeza kuwa “Hatua muhimu zimechukuliwa katika utekelezaji wa Mkataba wa mchakato wa amani, shukrani sana kwa uhamasishaji wa amani unaofanyika nchini DRC na dhamira iliyothibitishwa na viongozi wa nchi hiyo kukutana kwa pamoja kuzungumzia changamoto ambazo ni kikwazo cha kulitoa taifa hilo kwenye wimbi la machafuko.”
Kinachofanyika DRC
Mjumbe huyo amesema baada ya kuchukua madaraka, Rais wa DRC Felix Tshisekedi aliahidi kufanya kazi kwa karibu na wenzake kurejesha amani na usalama mashariki mwa DRC, mlango huu wa kidiplomasia ulikaribishwa na viongozi wote wan chi hiyo niliokutana nao ambao walinihakikishia kujitolea kwao kuunga mkono mchakato huo kwa ushirikiano.
Katika muktadha huu, mikutano ya pande tatu, ilifanyika kwamsaada wa ofisi ya Rais wa DRC na Rais wa Angola, msaada uliowezesha maelewano kati ya Uganda na Rwanda, na kusainiwa kwa Mkataba wa muafaka kati ya nchi hizi mbili ambazo ni ndugu, akiongeza kuwa “Ningependa kupongeza kujitolea kwa Serikali za Uganda na Rwanda ili kupunguza mvutano na kurudisha ushirikiano baina yao. Lazima pia niipongeze Angola na DRC kwa uamuzi wao wa kukuza mazungumzo na kudumisha azimio la amani na kuepusha mizozo katika maeneo ya Mashariki mwa DRC na nali ninaliomba Baraza lihimize muendelezo wa juhudi hizi.”
Mshikamano katika kudumisha usalama na amani
Bwana. Xia amegusia pia mchango wa ushirikiano wa mataifa jirani akisema Kujitolea kushirikiana katika ngazi ya usalama kulikodhihirika hivi karibuni kumesababisha mshikamano kati ya huduma za usalama na ulinzi za DRC na zile za nchi jirani, za Burundi, Uganda na Rwanda, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wao dhidi ya vikosi vyenye silaha mashariki mwa DRC. Hatua hizi zinaonyesha umuhimu wa mchakato wa jumla wa kikanda katika kukabiliana na tishio la usalama.
Hatua zilizochukuliwa hadi sasa
Mjumbe huyo maalum wa Maziwa Makuu amelieleza Baraza la Usalama kwamba “Kwa kuzingatia kile ambacho nimeweza kufanya hadi sasa, naweza kukuhakikishia kwamba kuna fursa muhimu ya kushughulikia sababu za kutokuwa na utulivu. Kwa hivyo, inapaswa kutia shile ili kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kuwezesha watu kufaidika vyema na utajiri wa nchi zao”.
Kufikia sasa, Xia amesema programu za maendeleo lazima ziimarishwe na ushirikiano wa kikanda lazima uharakishwe. Ni kwa kufahamu uhusiano uliopo kati ya kwa upande mmoja wa kuhakikishiwa amani na usalama na, upande mwingine, maendeleo ya pamoja na mafanikio ambayoyataleta mafanikio na mabadiliko katika taifa la DRC na kupunguza migogoro ambayo italeta utulivu katika kanda nzima.
Bado kuna changamoto Maziwa Makuu
Mbali ya mafanikio makubwa mjumbe huyo amekiri kwamba “ Kwa kweli, bado kuna changamoto nyingi zinaendelea. Ukosefu wa usalama unaotokana na uwepo wa makundi ya wanaharakati wenye silaha Mashariki mwa DRC, wa kigeni na wa ndani, hii bado ni shida kubwa. Ukiongeza na unyonyaji na biashara haramu ya maliasili ni vitu vinavyochochea kuendelea kwa uchumi haramu ambao unasaidia vikundi hivi vyenye silaha silahakuendelea kushamiri.”
.Ameongeza kuwa changamoto nyingine ni watu kuendelea kufaungasha virago na kukimbia makazi yao kwa sababu ya ukosefu wa usalama na ni jambo linaloonekana kuwa ni la kawaida. Kwa kuongezea, amesema “juhudi kubwa zinahitajika kulinda na kukuza haki za binadamu, kuhakikisha haki zaidi, usawa zaidi na heshima zaidi kwa hadhi ya mwanadamu.”
Mikakati ya ofisi ya mjumbe wa maziwa Makuu
Bawan. Xia amesema ofisi yake kwa kushirikiana na wadhamini wengine wa Mkataba wa mchakato wa amani, ili kusaidia nchi katika utiaji saini.
Kuhusu suala la ushirikiano wa usalama kwa ajili ya kupambana na waasi, wadhamini wa mkataba huo, pamoja na mfumo wa ufuatiliaji wa kitaifa nchini DRC, wanawezesha kufanyika kwa mashauriano kati ya wakuu wa huduma za ujasusi wa DRC, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na DRC. Uganda, Rwanda na Tanzania.
“Katika muktadha huu, Ofisi yangu imefanya mashauriano na nchi zinazohusika kuhusu hatua zisizo za kijeshi ambazo zinaweza kuambatana na shughuli za jeshi. Hata kama chaguo la kijeshi linabaki kuwa la muhimu, mipango ya lmuhimu lazima iwekwe, kwa msaada wa jamii ya kimataifa, ili kuwezesha usalimishaji wa silaha, na ujumuishaji wa vikundi katika nchi zao na ukarabati jamii"