Tunauteketeza mustakabali wetu:Bachelet

9 Septemba 2019

Baraza la haki za binadamu leo limefungua pazia mjini Geneva Uswis huku kamisha mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa akionya kwamba moto wa nyika unaoendelea kusambaa Amazoni “kimsingi tunautekeleza mustakabali wetu”.

Katika wito wake kwa nchi wanachama 47 wa Baraza hiliko akiwataka kuungana kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, Michelle Bachelet amesisitiza kwamba kila ukanda wa dunia hii ushikamane na waathirika.

Ameopngeza kuwa katika kipindi kifupi kumekuwa na athari kubwa za moto huo na kusambaratisha miti Bolivia, Paraguay na Brazil kwa familia ambazo zilikuwa zikiishi katika maeneo hayo. Amesisitiza kwamba “mabadiliko ya tabianchi ni  hali halisi ambayo sasa inaathiri kila pembe ya dunia na athari za matarajio la ongezeko la joto duniani kwa binadamu ni zahma kubwa. Vimbunga vinaongezeka na mawimbi ya bahari yanaweza kuzamisha visiwa na miji iliyoko pwani. Moro umetapakaa katika mistu yetu, na theluji inayeyuka, kimsingi tutauteketeza mustakabali wetu.”

Akikumbushia ripoti za Umoja wa Mataifa zisemazo kwamba dharura ya mabadiliko ya tabianchi imesababisha ongezeko kubwa la viwango vya njaa duniani , Kamishina Bachelet amesema , hali ya joto huenda ikaongezeka na huenda ikachangia vifo Zaidi 250,000 kwa mwaka kati ya mwaka 2030 na 2050 kutokana na utapiamlo, malaria, kuhara, na msongo utokanao na joto kali.

Ukumbi wa Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ambamo kwalo wataalamu wa haki za binadamu huchangia hoja kuhusu haki za binadamu
UN Photo - Jean-Marc Ferre
Ukumbi wa Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ambamo kwalo wataalamu wa haki za binadamu huchangia hoja kuhusu haki za binadamu

Hatujawahi kushuhudia tishio la kiwango hiki kwa haki za binadamu

Bi. Bachelet ameongeza kuwa “Dunia haijawahi kushuhudia asiliani tishio la kiwango hichi dhidi ya haki za binadamu . Hii sio hali ambayo nchi yotyote, taasisi yoyote, mtunga sera yeyote, anaweza kusimama kando. Uchumi wa mataifa yote, mfumo wa kisiasa , kiuchumi na kijamii wa kila taifa na haki za watu wenu wote  na mustakabali wa vizazi vijavyo utaathirika.”

Bachelet akizungumza siku 14 kabla ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

António Guterres kufungua mkutano wa kimataifa wa hatua kwa ajili ya mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, amelitaka Baraza la haki za binadamu kutimiza wajibu wao pia.

“Kila nchi inapaswa kuchangia kwa hatua zozote madhubuto zinazowezekana kuzuia mabadiliko ya tabia nchi. Ni lazima wachagize mnepo na haki za raia zao wakati wakitekeleza sera, pia ametoa msisitizo kuhusu suala la watu wa asili na  makundi ya walio wachache na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kunakopaswa kutupiwa jicho kuhusu haki

Kamishina mkuu pia amesema katika kuzingatia utamaduni kuna haki za kibinadamu katika baadhi ya nchi ambazo zinahitaji kutupiwa jicho na Baraza la haki za binadamu.

Ametoa mfano wa hofu kuhusu hali ya Kashmir ambako kumeelezwa amri ya kutotembea usiku inaendelea kutekelezwa huku mtandao wa intaneti ukifungwa na vizuizi kuwekwa dhidi ya mikusanyiko ikiwemo kuwasweka rumande wanaharakati wa haki za binadamu.

Bi. Bachelete ametoa wito kwa Pakistan na hususani kwa India kuhakikisha watu wanapata fursa ya huduma za msingi. Ametaja pia kuhusu zoezi la sensa ya hivi karibuni iliyofanyika katika nusu ya jimbo la Assan Kaskazini Mashariki mwa India.

Amesema watu milioni 1.9 hawakuhusishwa katika orodha hii , na ametoa wito kwa mamlaka ya India kuhakikisha mchakato unakamilika kwa kila mtu anayepnga mchakato huo na wakati huohuo kuhakikisha kwamba watu wanalindwa dhidi ya hali ya kutokuwa na utaifa.

Kubadilishana wafungwa Ukraine ni hatua kubwa

Akigusia hatua ya karibuni kuhusu Ukraine Bachelet amesema mahali ambako kwa zaidi ya miaka mitano ya machafuko katika eneo la Mashariki mpakani na Urusi kumewaacha maelfu ya watu wakipoteza Maisha na kujeruhiwa wengine maelfu kwa maelfu, anakaribisha muafaka wa kuachiliwa kwa wafungwa baiana ya nchi hizo mbili.

“Nazichagiza pande zote kuendeleza ari hiyo na kukomesha uhasama unaoendelea Mashariki mwa Ukraine”.

Akigeukia Afrika Kusini amesema anatambua kuhusu “matukio mabaya kabisa ya hivi karibuni ya ghasia za chuki dhidi ya wageni , ambapo mlolongo wa mashambulizi umeripotiwa mashambuzli ambayo yamekatili Maisha ya watu 10 raia wa kigeni nchini humo.

“watu wote Afrika Kusini , raia na wageni wako sawa , wanastahili haki za msingi za binadamu chini ya katiba na sharia za kimataifa za haki za binadamu.” Pia amekaribisha hatua ya Rais Cyril Ramaphosa ya kulaani vikali machafuko hayo.

Baraza jipya la mawaziri Sudan ni hatua ya kusherehekewa

Kuhusu Sudan ambako baraza jipya la mawaziri limeapishwa siku ya Jumapili likiwa ni la kwanza tangu kuondolewa madarakani kwa Rais Omar Al Bashir mwezi April baada ya maandamano makubwa nchi nzima, Bi. Bachelet ameiita hatua hiyo ni maendeleo makubwa na ni suala la kulisherehekea.

Pia amekaribisha vipengele kadhaa vya haki za binadamu vilivyojumuishwa kwenye azimio la katiba mpya ya nchi hiyo ikiwemo dhamira ya kuanzisha kamati ya kitaifa ya uchunguzi, kufuatia ripoti za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya waandamanaji.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter