Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna hatua iliyochukuliwa na India wala Pakistan kuimarisha haki za binadamu Kashmir:UN

Mwanamke akipita kwenye mpaka wa India na Kashmir katika mji wa Srinagar katika jimbo  la Jammu
Nimisha Jaiswal/IRIN
Mwanamke akipita kwenye mpaka wa India na Kashmir katika mji wa Srinagar katika jimbo la Jammu

Hakuna hatua iliyochukuliwa na India wala Pakistan kuimarisha haki za binadamu Kashmir:UN

Haki za binadamu

Ripoti ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo kuhusu hali ya haki za binadamu kwenye eneo la Kashmir upande wa India na Pakistan imesema idadi ya vifo vya raia na majeruhi iliyoripotiwa katika kipindi cha miezi 12 iliyopita ni ya juu zaidi kutokea kwa zaidi ya muongo mmoja na si India wala Pakistan waliochukua hatua Madhubuti kushughulikia masuala yanayotia haki kuhusu haki ambayo yaliainishwa na ripoti ya awali ya Umoja wa Mataifa

Ripoti hiyo mpya iliyochapishwa leo na ofisi ya Kamisha mkuu wa haki za binadamu imemulika kipindi cha Mei 2018 hadi Aprili 2019 na inatanabaisha jinsi gani mvutano dhidi ya Kashmir ulioongezeka baada ya shambulio la kujitoa muhanga la mwezi Februari likilenga vikosi vya usalama vya India kwenye eneo la Pulwama umeendelea kuathiri vibaya haki za binadamu za raia ikiwemo haki ya kuishi.

Idadi ya waliopoteza maisha

Kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa na asasi za kiraia za eneo hilo , ripoti inasema takribani “raia 160 waliuawa mwaka 2018 idadi inayosemekana kuwa ni kubwa zaidi katika kipindi cha muongo mmoja.Mwaka jana pia waliorodhesha idadi kubwa ya majeruhi yaliyotokana na mgogoro tangu mwaka 2008, huku watu 586 waliuawa wakiwemo wapiganaji wa makundi yenye silaha 267 na askari 159 wa vikosi vya usalama.

Ripoti inasema katika jumla ya vifo 160 vilivyoripotiwa , watu 71 wamedaiwa kuuawa na vikosi vya usalama vya India, 43 wadaiwa kuuawa  na makundi yenye silaha au watu wasiojulikana na 29 wamedaiwa kuuawa  kutokana na mguruneti na risari zilizokuwa zikufyatuliwa na vikosi vya usalama vya Pakistan katika eneo wanalolidhibiti la Kashmir.

Serikali ya Pakistan imesema watu wengine raia 35 zaidi waliuawa na 135 kujeruhiwa kwenye upande wa udhibiti wa Pakistan kutokana na makombora yaliyokuwa yakivurumishwa na vikosi vya India mwaka 2018.

Hali halisi inayoendelea

Makundi mawili yenye silaha yameshutumiwa kuingiza Watoto kwenye mapigano katika upande wa Kashmir unaodhibitiwa na india  na makundi hayo pia yanadaiwa kuhusika na mashambulizi dhidi ya watu walio na uhusiano au kushirikiana na mashirika ya kisiasa  katika neoe la Jammu na Kashmir, ikiwemo mauaji ya takriban watu 6 wafanyakazi wa vyama vya kisiasa  na viongozi waliojitenga.

Ripoti pia imeeleza kwamba upande wa Kashmir unaodhibitiwa na India uwajibikaji wa ukiukwaji wa uhalifu uliotekelezwa na vikosi vya usalama vya India haupo. Imeongeza kuwa licha ya idadi kubwa ya wraia waliouawa katika makabiliano baina ya vikosi vya usalama na makundi yenye silaha “hakuna taarifa zozote kuhusu uchunguzi wowote mpya wa matumizi ya nguvu kupita kiasi uliosababisha mauaji hayo na majeruhi.”

Ripoti pia inasema ofisi ya haki za binadamu “imepokea tarifa za uhakika kwamba watu wamekuwa wakitoweka katika eneo la Kashmir linalodhibitiwa na upande wa Pakistan ikiwemo wale waliokuwa wakishikiliwa rumande katika mahabusu za siri na wengine ambao hadi sasa mahali waliko imesalia kuwa kitendawili.”

Imetaja makundo manne yenye silaha ambayo yanaendelea na operesheni zake hivi sasa kwenye upande wa Kashmir unaodhibitiwa na India kuwa ni Lashkar-e-Tayyiba, Jaish-e-Mohammed, Hizbul Mujahideen na harakat Ul-Mijahidin yanaaminika kuwa na maskani yake kwenye upande unaodhibitiwa na Pakistan.

Ripoti hiyo imesisitiza kwamba “si serikali ya India wala ya Pakistan ambayo imechukua hatua za kushughulikia na kutekeleza mapendekezo ya yaliyotolewa na ripoti iliyopita ya ofisi ya haki za binadamu ambako ilichapishwa Juni 2018 hivyo inayarejerea mapendekezo hayo na kupendekeza uwezekano wa kuundwa tume ya uchunguzi ili kufanya uchuguzi huru wa kimataifa  dhidi ya madai ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu Kashmir.”

TAGS: Kasmir, India, Pakistan, OHCHR haki za binadamu