Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchunguzi dhidi ya ukiukwaji wa haki Kashmir lazima ufanyike:Zeid

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa , Zeid Ra'ad Al Hussein
Picha ya UN/Jean-Marc Ferré
Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa , Zeid Ra'ad Al Hussein

Uchunguzi dhidi ya ukiukwaji wa haki Kashmir lazima ufanyike:Zeid

Haki za binadamu

Miongo ya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa pande zote katika mgogoro wa Kashmir, umekatili na kusambaratisha maisha ya watu wengi na hivyo ni lazima kufanyike uchunguzi wa kina wa kimataifa amesema leo Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa.

Akizungumzia uzinduzi wa ripoti ya kwanza kabisa ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu kwa ajili ya Kashimir, eneo linalogombewa na kutenganisha baina ya India na Pakistan, Zeid Ra’ad Al Hussein ameelezea nia yake ya kuliomba Baraza la haki za binadamu  mjini Geneva kuunda tume ya uchunguzi katika kikao chake kijacho kitakachoanza Jumatatu.

Kamishina huyo Mkuu ambaye muda wake unamalizika majira haya ya kiangazi, ameainisha kile alichokiita “tatizo sugu la ukwepaji sheria kwa ukiukwaji unaotekelezwa na vikosi vya ulinzi “na kuongeza kwamba mfumo wa kisiasa wa mgogoro wenyewe umefunika “madhila yasiyoelezeka “ ya mamilioni ya watu.

Lengo kuu la ripoti hiyo yenye kurasa 49 “ni matumizi ya nguvu kupita kiasi” yanayofanywa na wanajeshi katika jimbo la Jammu na Kashmir, ingawa pia inatathimini ukiukwaji mwingine wa haki katika upande wa Kashimir unaodhibitiwa na Pakistan .

Katika upande wa Kashimir inayodhibitiwa na India, ripoti inaelezea ni jinsi gani kulizuka maandamano makubwa Jammu na Kashmir miaka miwili iliyopita, baada ya vikosi vya ulinzi vya India kumuua kiongozi wa kundi lenye silaha.

Inabainisha vipi nguvu kupita kiasi ilitumika  na kusababisha vifo vya takribani raia 145 kuanzia katikati ya mwaka 2016 hadi Aprili mwaka huu.

Jinsi waathirika wanavyokosa haki inasalia kuwa changamoto kubwa Jammu na Kashmir imeongeza ripoti hiyo. Pia imefafanua jinsi sheria inavyowapa wafanyakazi wa ulinzi kinga dhidi ya mkono wa sheria, mpaka pale tu serikali ya India itakaporuhusu na kusema hakujawahi kuwa na hukumu yoyote kwa takribani miaka 30 ambayo majeshi yenye silaha (Jammu na Kashmir) yamekuwa na mamlaka.

Ripoti imesisitiza “ukwepaji sheria huu”pia umezuia kuwepo kwa uchunguzi dhidi ya watu kutoweshwa au kutoweka, ikisonta kidole madai ya kuwepo makaburi ya pamoja katika jimbo hilo na madai ya ubakaji wa wanawake 23 uliofanywa na wanajeshi katika eneo la Kunan-Poshpora yapata miongo mitatu iliyopita.

Ikigeukia upande wa Kashmir inayodhibitiwa na Pakistan, ripoti hiyo ya ofisi ya haki za binadamu imeelezea ukiukwaji wa haki za binadamu upande huo kama ni wa aina au ukubwa tofauti.

Kwa kina imebainisha vikwazo vya uhuru wa kujieleza na haki za watu za kukusanyika kwa amani katika maeneo mawili ya azad Jammu na Kashmir (AJK) na Gilgit-Baltistan na kutaja hofu yake kuhusu ufafanuzi wa ugaidi, huku kukiwa na ripoti kwamba mamia ya watu wamekamatwa chini ya sheria za Pakistan za kupambana na ugaidi katika mji wa Gilgit-Baltis pekee.

Kamishina Mkuu zeid amesisitiza kuwa suluhisho lolote la kisiasa kwa upande wa Kashimir inayodhibitiwa na India na Kashmir inayodhibitiwa na Pakistan “ni lazima lijumuishe ahadi ya kukomesha mzunguko wa machafuko na kuhakikisha uwajibikaji kwa ukiukwaji uliofanywa na pande zote siku za nyuma na sasa.