Katibu Mkuu wa UN akaribisha kutiwa saini makubaliano kati ya Uganda na Rwanda

23 Agosti 2019

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekaribisha utiaji saini makubaliano tarehe 21 Agosti 2019 huko Luanda, Angola kati ya marais Yoweri Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda kwa minajili ya kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Amezishauri pande zote kutekeleza makubalano hayo kwa moyo mzuri, kwa lengo la kurejesha urafiki na ushirikiano kati ya majirani hao wawili kwa manufaa ya amani, uthabiti na maendeleo ya kudumu katika kanda hiyo.

Katibu mkuu anatambua umuhimu wa wajibu wa marais Joao Lourenco wa Angola na Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo kwa kuongoza kusainiwa makubaliano hayo.

Katibu mkuu yuko tayari kuunga mkono makubaliano hayo na yale yatafuatia na mipango mingine ya kuleta amani, ushirikiano na uwiano katika eneo hilo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud