Yoweri Kaguta Museveni

Balozi Philip Ochen Odida, Naibu Mwakilishi wa kudumu wa Uganda katika Umoja wa Mataifa akihutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA75
UN Photo/Loey Felipe

COVID-19 imetupa mafunzo-Uganda 

Tunauona ushirikiano wa kimataifa kama njia ya kushughulikia matishio magumu na mapya kama vile janga la COVID-19 ambalo limeathiri kila mwanachama wa jumuiya ya kimataifa, imeeleza sehemu ya kwanza ya hotuba ya Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda katika mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambayo imesomwa kwa niaba yake na Naibu Mwakilishi wa kudumu wa Uganda katika Umoja wa Mataifa, Balozi Philip Ochen Odida ikieleza pamoja na mengine, kile ambacho wamejifunza kutokana na ugonjwa huo. 

©UNICEF/Leonardo Fernandez

Uganda yajihadhari kabla ya shari ya COVID-19

Serikali ya Uganda imechukua hatua ya kufunga shule zote, masoko na mijumuiko yote ya umma kama mojawapo ya njia za kuzuia kuenea kwa virusi vya corona au COVID-19 kwenye nchi hiyo ambayo yenyewe hadi sasa haina mgonjwa hata mmoja lakini imezungukwa na nchi mlimothibitishwa mlipuko wa virusi hivyo.  Kutoka Uganda mwandishi wetu John Kibego anaripoti zaidi.

Hiyo ni sauti ya Rais Wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museveni akihutubia taifa kuhusu tishio la mlipuko wa virusi hatari vya COVID-19 akiwa kwenye ikulu ya Entebbe.

Sauti
2'24"