Dola milioni 50 zahitajika haraka kwa ajili ya vita dhidi ya Ebola DRC na nchi jirani-WFP

26 Julai 2019

Jumla ya dola milioni 50 zinahitajika hraka ili shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP liweze kufanya maandalizi muhimu kwa ajili ya kukabiliana na mlipuko wa Ebola unaoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na uwezekano wa mlipuko katika nchi jirani.

Katika taarifa yake iliyotolewa leo mjini Geneva Uswis WFP inasema fedha hizo ni kwa ajili ya kununua chakula cha msaada ambacho kinapangwa kugawanywa Disemba kinachopaswa kununuliwa sasa na pia maandalizi katika nchi jirani za

Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini katika miezi sita ijayo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva mwandihi wa WFP Herve Verhoosel amesema ikiwa ni mwaka mmoja tangu mlipuko wa kwanza wa Ebola kutangazwa DRC na iku 10 tangu kisa kuzuka Goma WFP inaongeza juhudi zake za misaada na maandalizi sababu ya uwezekano wa kusambaa kwa ugonjwa huo na kwamba

(SAUTI YA HERVE VERHOOSEL)

“Katika miezi sita ijayo WFP inapanga kuongeza karibu mara mbili msaada wa chakula na lishe kwa watu 440,000 walioathirika na Ebola DRC hussusan wale waliohusiana na waathirika na family zao pamoja na wale waliothibitishwa na washukiwa wa Ebola.”

 Ameongeza kuwa kufanya hivyo ni muhimu kwa ajili ya kupunguza maambukizi, watu kutoka sehemu moja kwenda kwingine ili kuambukiza na pia ni muhimu sana kwa ajili ya kamoeni ya chanjo inayoendelea.

Kwa sasa mgao huo wa WFP unafanywa katika maeneo ya makubaliano tu kwa wale wamaohusiana na waathirika na wahusika wapya wanakadiriwa kuwa takribani 50 kwa kila kisa hivyo kwa miei mitano ijayo inakadiriwa watu 75,000 wanaweza kuwa wamehusina kwa njia moja au nyingine na waathirika wa Ebola.

Na mgao huo wa chakula unagawiwa katika kaya za watu watanowatano na hupew mgao wa wiki moja moja mara nne kwa mwezi na hii inasaidia wao kurejea kituoni ambako wahuumu wa afya wa serikali na wale wa shirika la afya duniani pia huwafanyia uchunguzi wa afya zao

Mbali ya mgao wa chakula WFP imeongeza safari za ndege zake kwa ajili ya kampeni ya kupambana na Ebola na kuna vituo 69 ambayo vimewekwa tayari na shirika hilo katika maeneo makubwa ya mpakani kwa ajili ya uchunguzi wa Ebola na kugawa msaada unaohitajika.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter