Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali tete ya usalama imewalazimu maelfu kuwa wakimbizi wa ndani CAR:OCHA

Kinamama na watoto wakimbizi wa ndani katika kituo kimoja mjini Paoua, CAR
Yaye Nabo Sène/OCHA
Kinamama na watoto wakimbizi wa ndani katika kituo kimoja mjini Paoua, CAR

Hali tete ya usalama imewalazimu maelfu kuwa wakimbizi wa ndani CAR:OCHA

Wahamiaji na Wakimbizi

Maelfu ya watu wamesalia kuwa wakimbizi ama wakimbizi wa ndani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR na hawawezi kurejea makao kutokana na hali tete ya usalama inayoendelea.

Wakati dunia leo ikiadhimisha siku ya wakimbizi leo, watu 21,000 wamelazimika kukaa hapa kwenye kambi za Lazare na Mbella zinazohifadhi wakimbizi wa ndani na kusimamiwa na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini CAR ujulikanao kama MINUSCA .

Asilimia kubwa ya wakimbizi hawa wanatoka katika mji wa Kaga Bandoro na kurejea makwao hadi sasa imesalia kuwa ndoto limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharira OCHA.

Shirika hilo linasema robo ya watu wote wa CAR wametawanywa na machafuko na kuishia kuwa wakimbizi au wakimbizi wa ndani. Akiwa katika moja ya kambi hizo mkuu wa ofisi ya OCHA nchini CAR Francois Batalingaya anasema

SAUTI YA FRANCOIS BATALINGAYA

Hapa kaga Bandoro tuna wakimbizi wa ndani 21,500 wanaoshi kambini , pia tuna watu wengine 21,000 wanaohifadhiwa na familia za wenyeji na wote wanahitaji msaada wa kibinadamu.”

Ameongeza kuwa

SAUTI YA FRANCOIS BATALINGAYA 

Hii ni zahma kubwa na wanawake na wasichana bado wanabakwa huku ukatili wa kijinsia ukigeuzwa mazoea katika nchi hii”.

Prudence Tissara ni miongoni mwa wakimbizi wa ndani kambini hapo

SAUTI YA PRUDENCE TISSARA

“Tunakabiliwa na matatizo mengi katika kambi hii, kwa sababu bado tuko hapa tangu tulipokimbia, machafuko yanafanywa dhidi ya kaka na dada zetu. Tunauwa kaka zetu na kubaka dada zetu tunakabiliwa na changamoto nyingi”Tunataka amani irejee ili tuweze kuishi kama mwanzo, tunapokea mgao wa chakula lakini hautoshelezi”

OCHA inasema kwa mwaka huu peke wa 2019 watu milioni 2.9 CAR wanahitaji msaada wa kibinadamu na fedha zinazohitajika kupitia mfuko wa msaada wa kibinadu nchini CAR uitwao  HF umefadhiliwa kwa kiasi kidogo tu.