Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mlinda amani mtanzania aliyeokolewa na Chitete azungumza

Koplo Ali Khamis Omary ni mlinda amani mtanzania aliyeokolewa na mlinda amani marehemu Chancy Chitete kutoka Malawi ambapo akihojiwa na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
UNIC Dar es salaam

Amani na Usalama

Koplo Ali Khamis Omary ni mlinda amani, Komandoo mtanzania aliyeokolewa na mlinda amani marehemu Chau ncy Chitete kutoka Malawi ambapo akihojiwa na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam hii leo ameeleza kusikitishwa na kifo cha mwenzake na anaanza kwa kueleza tukio lilivyotokea.

Koplo Omary alianza kwa kuelezea kile ambacho kilitokea tarehe 14 mwezi Novemba mwaka 2018 huko Kididiwe jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, “nakumbuka mnamo tarehe 14 Novemba (2018) tulipokea jukumu la kwenda kwenye kambi ya Naru, Kididiwe, tulikuwa na askari wa Malawi. Katika jukumu hilo yalitokea mapigano makali nikapigwa risasi ya mguu, nashukuru nilikuwa karibu na private Chitete, kweli akanifunga mguu, baada ya kunifunga bandeji mguuni tukiwa tunaendelea na mapambano, baada ya muda nikamkuta mwenzangu amefariki.”

Kisha Koplo Omary akamtakia Chitete kupumzika kwa amani, “kwa kweli nimejisikia vibaya sana kwa kuwa yule ni mlinda amani mwenzangu ambaye tulikuwa tunashirikiana naye majukumu na sikupenda itokee hivyo ila Mungu ndiye amependa hivyo, namwombea sana kwa mungu.”