UN yakumbuka wafanyakazi wake waliofariki dunia kwenye ajali ya ndege Ethiopia

15 Machi 2019

Hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika tukio maalum la kukumbuka wafanyakazi 21 wa umoja huo waliofariki dunia kwenye ajali  ya ndege ya shirika la ndege la Ethiopia, iliyotokea huko Addis Ababa Ethiopia Jumapili iliyopita.

Tukio hilo limeongezwa na Katibu Mkuu António Guterres ambapo ameweka shada la maua kwenye dirisha maalum la kumbukizi ndani ya jengo la makao makuu ya Umoja huo.

Akizungumza, Katibu Mkuu amesema, “wafanyakazi wenzetu walikuwa ni kundi lililojumuisha watu kutoka pande mbalimbali. Walikuwa wanatoka kwenye mashirika, wengi wakiwa na utaalamu wa hali ya juu kutoka ngazi mbalimbali za vyeo, na majukumu mbalimbali ndani ya Umoja wa Mataifa, wakitoka pande mbalimbali za dunia. Na bado, pamoja, wao pia walikuwa ndio taswira ya Umoja wa Mataifa: Hakika waliwakilisha kile ambacho Umoja wa Mataifa ni nini? Na Umoja wa Mataifa bora.”

Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa waliouawa kwenye ajali ya ndege ya shirika la ndege la Ethiopia huko Addis Ababa, wamekumbukwa leo 15 Machi 2019  kwenye makao makuu ya UN.
UN /Manuel Elias
Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa waliouawa kwenye ajali ya ndege ya shirika la ndege la Ethiopia huko Addis Ababa, wamekumbukwa leo 15 Machi 2019 kwenye makao makuu ya UN.

Ndege hiyo ya Ethiopia namba ET 302 ilianguka Jumapili na kuua watu wote 157 waliokuwemo.

Kwa mujibu wa wa takwimu zilizotolewa na shirika hilo, raia wenye utaifa kutoka nchi 35 walikuwemo kwenye ndege hiyo aina ya Being 737 iliyokuwa inaelekea mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Wafanyakazi hao ni Joanna Toole, Anne Feigl, Maygenet Worku Abebe Marcelino Tayob, Shikha Garg, Victor Shing Ngai Tsang, Nadia Adam Abaker Ali, Jessica Hyba , Jackson Musoni, Susan Mohamed Abufarag , Graziella De , Esmat Adelsattar Taha , Oliver Vick, Max Thabiso Edkins, Ekta Adhikari, Maria Pilar Buzzetti, Virginia Chimenti, Harina Hafitz, Zhen-Zhen Huang, Michael Eoghan Ryan, na Djordje Vdovic. 

 

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter